Taarifa mpya ya COVID-19: Vifo viwili vipya vya COVID-19 vya rekodiwa NSW

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia ya 25 Julai 2021.

Kiongozi wa NSW Gladys Berejiklian atoa taarifa mpya kuhusu COVID-19 mjini Sydney.

Kiongozi wa NSW Gladys Berejiklian atoa taarifa mpya kuhusu COVID-19 mjini Sydney, Jumapili, 25 Julai, 2021. Source: AAP Image/Lisa Maree Williams

  • NSW yarekodi vifo viwili kutoka COVID-19.  
  • Kesi zote jimboni Victoria zina ungwa kwa mlipuko wa sasa. 
  • Serikali ya Shirikisho yapata dozi milioni 85 za ziada za Pfizer.
  • Hatua zaku inua makatazo ya Kusini Australia zaendelea vizuri. 

New South Wales

NSW imerekodi kesi mpya 141 ndani ya jamii. Watu wawili wamefariki, mwamke mmoja katika miaka ya sabini, na mwanamke mmoja katika miaka ya 30 ambao hawakuwa na magonjwa sugu, kiongozi wa NSW Berejikilian amesema. 

NSW itapokea dozi za ziada za COVID-19 elfu 50,000 za Pfizer. Wakati huo huo, kitengo maalum cha polisi kime undwa kuwatambua watu walio shiriki katika maandamano ya jana, hati za adhabu 510 zikiwa zimetolewa tayari.

Pata hapa katika orodha au ramani.

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 11 ndani ya jamii, zote zilikuwa ndani ya karantini katika wakati wote ambao zilikuwa katika hali ambukizi na, zina ungwa kwa mlipuko wa sasa.

Mamlaka bado hawaja thibitisha hatua zaku regezwa kwa vizuizi vya COVID-19 Jumanne 27 Julai 2021.

Pata hapa, kwenye orodha au ramani.

Hali ilivyo kuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita

  • Australia itapokea dozi za chanjo ya COVID-19 milioni 85 za Pfizer katika miaka ya 2022 na 2023.
  • Kusini Australia imerekodi kesi mpya tatu ndani ya jamii, na bado jimbo hilo liko katika mwelekeo waku inua makatazo.  
  • Queensland imerekodi kesi mpya tano ndani ya karantini ya hoteli.

Taarifa potovu kuhusu COVID-19:
Vijana wenye afya nzuri hawa athiriwi na COVID-19. Ina waathiri nakuwaua tu wazee au wagonjwa.

Ukweli kuhusu COVID-19:
Virusi hivyo huwa athiri wazee na wale ambao wana magonjwa sugu zaidi ila pia, vina waathiri nakuwaua baadhi ya vijana ambao wana afya nzuri.


Karantini, usafiri, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Masharti ya karantini na vipimo yana simamiwa na kutekelezwa na serikali za majimbo na mikoa:


ACT  na 
QLD  na 
TAS  na 
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza wasilisha ombi lako mtandaoni.  kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia.

 

Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo, huwa zina tathminiwa kila mara na serikali na, taarifa mpya kuchapishwa kwenye tovuti ya .





Tembelea shirika la NSW Multicultural Health Communication Service kwa huduma zilizo tafsiriwa:

Zahanati za vipimo katika kila jimbo na mkoa:


 
 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo na mkoa:

 
 

Share
Published 25 July 2021 4:15pm
Updated 12 August 2022 3:06pm
By Gode Migerano, SBS/ALC Content
Presented by SBS/ALC Content, Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends