Taarifa mpya ya UVIKO-19: TGA yatathmini usahihi wa vipimo vya UVIKO wakati idadi ya wanao lazwa hospitalini yaongezeka sana

Hii ni taarifa yako mpya ya UVIKO-19 nchini Australia kwa 26 Julai.

Healthcare workers administer COVID-19 tests at the St Vincent's Hospital drive-through testing clinic.

Healthcare workers administer COVID-19 tests at the St Vincent's Hospital drive-through testing clinic. (file) Source: (AAP Image/Bianca De Marchi)

Jumanne, Australia iliripoti vifo 75 vya UVIKO-19, vifo 26 viki ripotiwa New South Wales (NSW), 25 Victoria na 18 Queensland.

Queensland iliripoti watu 983 ambao wamelazwa hospitalini kwa UVIKO-19 - hiyo ikiwa ni idadi kubwa zaidi tangu janga lilipo anza. 

Tazama maendeleo mapya ya UVIKO-19 kwa kesi mpya, wanao lazwa hospitalini na vifo nchini Australia .


Utawala wa Bidhaa za Tiba (TGA) imetoa idhini ya muda chanjo ya Moderna ya Spikevax kwa watoto wenye kati ya umri wa miezi sita na miaka mitano. Dozi hizo mbili zinaweza tolewa siku 28 baada ya moja kutolewa.

"Majaribio ya zahanati yameonesha kuwa hali ya usalama wa watoto ni sawia na ule ulio onekana katika watu wazima. Matukio mabaya zaidi yalishuhudiwa katika majaribio ya zahanati katika watoto wenye umri wa miezi sita hadi miaka misita, baadhi ikiwa kidogo au wastan kwa ujumla baada ya dozi ya pili kutolewa," alisema. 

"Motokeo haya yana husu kuwashwa/kulia, wekundu na au kuvimba sehemu mtu alipo dungwa sindano, uchovu, homa, maumivu ya misuli na uvimbe karibu ya sehemu ya siri pamoja na ulegevu."

Hatahivyo, chanjo bado inahitaji idhinishwa na Kundi la Ushauri wakiufundi la Australia kwa chanjo (ATAGI), kabla itumiwe na watoto.  

Jumanne, ATAGI ilipendekeza kupunguza muda wa sasa wa kati ya utoaji wa dozi ya nne na, maambukizi ya sasa ya coronavirus kuanzia miezi minne hadi miezi mitatu.  

ATAGI imesema ufunikaji wa juu wa dozi za jeki za UVIKO-19 katika majira ya baridi, katika watu wazima wenye kati ya miaka 50-64 wakijumuishwa, inaweza punguza idadi ya wanao lazwa hospitalini kwa coronavirus katika miezi ijayo.

Waziri wa huduma za serikali Bill Shorten, amewaomba wafanyakazi watumie likizo zao za wagonjwa, kabla yakudai malipo ya janga.

Nao mamlaka wa Afya na shule kote nchini Australia, wana wahamasisha wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa shule wavae barakoa angalau kwa wiki za kwanza nne za mhula wa tatu.

NSW inaweza wasilisha tena kwa muda hatua za ziada kwa shule zake.

Hatua hizi zinajumuisha kusitisha mikusanyiko ya watu wengi katika sehemu za ndani, kusitisha matukio ya ndani ya kati ya shule na nyingine, kufuta au kuahirisha matukio yakukesha pamoja na ziara.

Pamoja nakuweka masharti yakuvaa barakoa kwa watu wazima na wanafunzi wa shule za sekondari, kuzuia idadi ya wageni katika shule, kutenga baadhi ya wanafunzi, kusomea nyumbani au katika sehemu nyingine na watu wa karibu kuhudhuria shule.

Waziri wa huduma ya wazee Anika Wells, amesema idara yake itachapisha viwango vya wakaaji ambao wamepata chanjo katika makaazi binafsi ya huduma ya wazee kuanzia 1 Agosti.  

 


 




Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19

Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya 



Kama unahitaji msaada wa fedha, 

Hapa kuna msaada waku saidia kuelewa 



Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika Kiswahili kwenye.  


Share
Published 26 July 2022 2:34pm
Presented by Gode Migerano


Share this with family and friends