Taarifa mpya ya UVIKO-19: TGA yatoa idhini ya chanjo ya watoto wenye chini ya miaka mitano; wanafunzi wahamasishwa wavae barakoa

Hii ni taarifa yako mpya ya UVIKO-19 nchini Australia kwa 19 Julai.

Authorities in the US and Canada have already approved Moderna's Spikevax vaccine in children under five. (file)

Authorities in the US and Canada have already approved Moderna's Spikevax vaccine in children under five. (file) Source: AAP/AP/zz/STRF/STAR MAX/IPx

Jumanne, Australia iliripoti vifo 75 vya UVIKO-19, vikijumuisha 26 New South Wales (NSW), 25 Victoria na 18 Queensland.

Queensland iliripoti watu 983 walio lazwa hospitalini wakiwa na UVIKO-19, hiyo ikiwa ni takwimu kubwa zaidi tangu janga lilipo anza. 

Tazama maendeleo ya kesi mpya za UVIKO-19, wanao lazwa hospitalini na vifo nchini Australia .


Utawala wa Bidhaa za TIba (TGA) imetoa idhini kwa muda kwa matumizi ya chanjo ya Moderna Spikevax kwa watoto wenye umri wa miezi sita hadi miaka mitano. Dozi hizo mbili zinaweza tolewa siku 28 baada ya dozi ya kwanza kutolewa.

"Majaribio yazahanati yalionesha kuwa usalama wa watoto ni sawia na ule unao onekana katika watu wazima. Matukio mabaya yaliyo shuhudiwa katika majaribio ya zahanati katika watoto wenye umri wa miezi sita hadi miaka sita, yalikuwa wastan na kwa ujumla yaliripotiwa baada ya dozi ya pili" kutolewa taarifa hiyo ilisema. 

"Hizi ni pamoja nakuwashwa/kulia, rangi nyekundu kuonekana kwenye mwili/au kuvimba sehemu alipodungwa sindano, mchoko, homa, maumivu ya misuli pamoja nakuvimba katika sehemu za siri."

Hata hivyo, chanjo hiyo bado lazima ipewe idhini na kundi lakiufundi la ushauri wa Australia kwa chanjo (ATAGI) kabla itumiwe ndani ya watoto.  

Jumanne, ATAGI imependekeza kupunguzwa kwa muda kati ya dozi za nne zinazo tolewa na maambukizi ya coronavirus ya hivi karibuni, kutoka miezi minne hadi miezi mitatu.

ATAGI amesema utoaji mkubwa wa dozi ya jeki UVIKO-19 ya msimu wa majira ya baridi kwa watu wazima, watu wenye miaka 50 hadi 64 wakijumuishwa, inaweza punguza idadi ya wanao lazwa kwa coronavirus hospitalini katika miezi ijayo. 

Waziri wa Huduma za Serikali Bill Shorten aliwaomba wafanyakazi watumie likizo zao za wagonjwa, kabla yakudai malipo ya janga.

Mamlaka wa Afya na shule kote nchini Australia, wana wahamasisha wanafunzi na wafanyakazi wa shule wavae barakoa angalau kwa wiki nne za kwanza za mhula wa tatu

NSW inaweza wasilisha kwa muda hatua za ziada katika shule.

Hatua hizo zinajumuisha kusitisha mikusanyiko ya vikundi vya watu wengi, kusitishwa kwa matukio ya nje na kati ya shule, kufutwa au kuahirishwa kwa kwa matukio na safari za shule.

Na kuweka amri yakuvaa barakoa kwa watu wazima na wanafunzi wa shule la upili, kupunguza ziadra katika shule, kutenganya wanafunzi, kusomea nyumbani au sehemu nyingine pamoja na kujumuika kwa karibu shuleni.

Waziri wa Huduma ya Wazee Anika Wells, amesema idara yake itachapisha viwango vya chanjo vya wakaaji ndani ya makaazi binafsi ya huduma ya wazee kuanzia 1 Agosti.  

 


 





Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19

Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya 



Kama unahitaji msaada wa fedha, 

Hapa kuna msaada waku saidia kuelewa 



Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika Kiswahili kwenye.  


Share
Published 19 July 2022 2:30pm
Presented by Gode Migerano


Share this with family and friends