- Queensland yarekodi kesi mpya tisa za COVID-19 ndani ya jamii
- Cairns na Yarrabah zaingia katika siku tatu za vizuizi kuanzia saa 10 jioni ya leo
- Kifo kimoja na kesi mpya 262 za COVID-19 zimerekodiwa leo jimboni NSW
- Victoria yaripoti kesi mpya 11 za COVID-19 ndani ya jamii
Queensland
Queensland imeripoti kesi mpya tisa ndani ya jamii. Kesi saba zina ungwa na mlipuko wa Indooroopilly, moja iko Gold Coast na kesi moja mpya iko Cairns.
Makatazo katika eneo la Kusini Mashariki Queensland, yata isha kama ilivyo ratibiwa leo saa kumi mchana ila, baadhi ya vizuizi vitasalia kwa muda wa wiki mbili zijazo, matumizi ya lazima ya barakoa yakijumuishwa.
Kiongozi wa Queensland Annastacia Palaszczuk amesema kesi hiyo mjini Cairns ina zua wasiwasi kwa sababu mhusika alifanya kazi kama dereva wa texi na, amekuwa katika hali ambukizi ndani ya jamii kwa siku 10.
Matokeo yake ni kwamba maeneo ya halmashauri yakanda ya Cairns pamoja na Halmashauri ya Yarrabah Aboriginal Shire Council yata ingia katika makatazo ya siku tatu, kuanzia saa kumi mchana wa leo.
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 262 za coronavirus ndani ya jamii, na mwanamke mmoja katika miaka ya themanini ame fariki.
Angalau kesi 72 katika kesi hizo mpya, zilikuwa ndani ya jamii wakati zilikuwa katika hali ambukizi.
Kiongozi wa NSW Gladys Berejiklian amesema vitongoji 12 katika halmashauri ya jiji la Penrith, vitawekwa kwenye orodha kama sehemu za wasiwasi na, vitawekewa vizuizi vya ziada kuanzia saa kumi na moja jioni ya Jumapili.
Victoria
Jimbo la Victoria limerekodi kesi mpya 11 za COVID-19 ndani ya jamii, kesi hizo zime ungwa na mlipuko wa sasa. Kesi hizo zote hazikuwa ndani ya karantini wakati zilikuwa katika hali ambukizi.
Wakaaji wa Victoria wenye kati ya miaka 18 na 39, wata weza pokea chanjo ya COVID-19 ya AstraZeneca katika vituo maalum vya chanjo kuanzia kesho Jumatatu.
Kituo cha kwanza chakutolea chanjo watu wakiwa ndani ya magari yao nchini Australia, kitafunguliwa jimboni Victoria katika jengo ambalo lili wahi kuwa duka la Bunnings, katika kitongoji cha Melton kuanzia kesho Jumatatu.
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga pandemic disaster payment
Karantini na masharti ya vipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na mikoa:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za muda kwa safari zakimataifa, ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, na taarifa hiyo huchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60 hapa
- Pata miongozo inayo faa kwa jimbo na mkoa wako: , , , , , , .
- Pata taarifa kuhusu
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa nakuchapishwa na huduma ya mawasiliano ya idara ya afya ya tamaduni mbali mbali ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na mkoa:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo na mkoa: