Latest

Taarifa mpya ya UVIKO-19: SA na ACT zaregeza vizuizi hospitalini, na katika makaazi ya huduma ya wazee

Hii ni taarifa yako mpya kuhusu UVIKO-19 nchini Australia kwa 26 Septemba.

MELBOURNE DAILY LIFE

South Australians are no longer required to check in on the mySAGOV app for visiting hospitals, aged care facilities, residential disability facilities and prisons. (file) Source: AAP / MORGAN HANCOCK/AAPIMAGE

Key Points
  • South Australia scraps check-in requirements at hospitals and prisons
  • Queensland reported a new monkeypox infection over the weekend
  • Pfizer CEO Albert Bourla again tests positive to COVID-19
Wilaya ya Australian Capital Territory (ACT) imeregeza vizuizi kwa wageni katika hospitali kuanzia leo.

Hatua hiyo itaruhusu idadi ya wageni zaidi ya mbili kuingia hospitalini kila siku. Hata hivyo, wageni wata takiwa kufuata vikomo vya mkusanyiko wa watu pamoja na hatua zingine za usalama ndani ya hospitali husika.

Wakaazi wa Kusini Australian wanao watembelea wakaazi ndani ya makaazi ya huduma ya wazee, hawata takiwa tena kuwa wamepata chanjo ya mafua au UVIKO-19.

Hata hivyo, lazima wavae barakoa.

Haitakuwa lazima tena kwa wakaazi nao kujisajili kwenye app ya mySAGOV, kutumbelea hospitali, makaazi ya huduma ya wazee, makaazi ya huduma ya walemavu namagereza.
Data mpya imeonesha kuna kesi 1,274 za UVIKO-19 katika milipuko 219 ndani ya makaazi ya huduma ya wazee kote nchini Australia.

NSW imeripoti kesi 67 za milipuko na inafuatwa na Victoria (66), Queensland (27), Magharibi Australia (25), Kusini Australia (25), Tasmania (4), Wilaya ya Kaskazini (3) na ACT (2).

Queensland iliripoti kesi mpya ya monkeypox (MPX) wikendi iliyopita, hali ambayo imefikisha idadi kamili ya maambukizi nchini kuwa zaidi ya 135.

Jimbo la Victoria (67) na NSW (52) hayo ni majimbo mawili yenye idadi kubwa ya kesi za maambukizi ya monkeypox (MPX ) nchini.
Albert Bourla ndiye mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya chanjo ya Pfizer, amepatwa na UVIKO-19 kwa maranyingine kwa mujibu wa taarifa kutoka kampuni hiyo.

Imeripotiwa kuwa Bw Bourla anajihisi vizuri, na hana dalili zozote za ugonjwa huo.

"Sijapata jeki mpya bado kwa sababu nilikuwa nikifuatilia mwongozo wa CDC, kusubiri kwa miezi mitatu tangu kesi yangu ya nyuma ya UVIKO, ambayo ilikuwa katikati ya Agosti," Bw Boural aliandika kwenye twitter.

"Wakati tumekuwa na maendeleo mengi, virusi bado viko nasi."

Pata hapa zahanati ya muda mrefu ya UVIKO

Pata hapa zahanati yakupimia UVIKO-19

Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya

Kabla uende ng'ambo, Hapa kuna msaada waku kusaidia kuelewa Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika lugha yako

Share
Published 27 September 2022 4:21pm
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends