- Kiongozi wa NSW atangaza kuregezwa kwa vizuizi katika halmashauri za jiji zenye wasi wasi.
- Victoria yatoa mwongozo wakufungua jimbo tena
- ACT yaripoti kesi mpya 17 za COVID-19 ndani ya jamii
- Queensland yaweka rekodi mpya ya chanjo nyingi zaidi katika siku moja
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 1,083 za maambukizi ndani ya jamii, pamoja na vifo 13.
Kiongozi wa jimbo hilo Gladys Berejiklian alitangaza kuwa kuanzia Jumatatu 20 Septemba, sehemu zote za wasiwasi zitakuwa na , ila masharti yawafanyakazi wanao ruhusiwa pamoja na masharti ya vibali vya usafiri vitasalia.
Sehemu za kuogoela za nje kote jimboni NSW, zitafunguliwa kuanzia Jumatatu 27 Septemba, kama zitakuwa na mpango salama wa COVID unao idhinishwa.
Kwa sasa 81.9% ya wakaaji wa NSW wanao stahiki, wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo na 51.9% ya wakaaji wame pokea chanjo kamili.
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 507 ndani ya jamii, pamoja na kifo kimoja.
Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews aliweka wazi mchakato wenye hatua tano zakuondoa jimbo hilo ndani ya vizuizi. Makatazo yata isha wakati 70% ya umma wa jimbo hilo wanao stahiki wame pata chanjo kamili, hatua ambayo inatarajiwa itakamilika tarehe 26 Oktoba. “Tuna fungua tena, na hapatakuwa kurudi nyuma” Bw Andrews alisema. Kufikia siku ya krismasi, idadi ya wageni 30 wata ruhusiwa ndani ya nyumba moja, kama viwango vya 80% vya chanjo vina timizwa.
Data inaonesha angalau 71.2% ya watu wa Victoria wanao stahiki, wamepokea angalau dozi moja ya chanjo ya COVID-19 na, 43.5% yao wame pokea chanjo kamili.
Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24
- ACT imerekodi kesi mpya 17 za maambukizi, 12 kati yazo zilikuwa katika hali ambukizi ndani ya jamii kwa muda.
- Idadi ya watu 31,004 wa Queensland walichanjwa jana, hiyo ikiwa ni rekodi kwa jimbo hilo. 59.34% yawatu kwa sasa wame pata tayari dozi yao ya kwanza.
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: