Jumanne, Australia iliripoti vifo 37 vya UVIKO-19, ambavyo vilijumuisha vifo 11 jimboni New South Wales, 12 Victoria, 6 Queensland na 6 Kusini Australia, na 2 Tasmania. Magharibi Australia iliripoti pia vifo vitatu vyakihistoria.
Idadi ya watu wanao lazwa hospitalini jimboni Queensland imekuwa ikiongezeka katika miezi iliyopita. 12 Aprili, watu 572 walikuwa hospitalini kulinganisha na watu 247 mwezi uliopita.
Serikali ya Australia itatoa dawa ya pili ya ambayo daktari lazima atoe kwa mgonjwa, na itatolewa kupitia mfumo wa faida ya mandawa (PBS) kwa wa Australia ambao wako katika hatari ya juu yakupata aina mbaya ya UVIKO-19 kuanzia 1 Mei 2022.
Wagonjwa wenye kiwango kidogo au wastan cha UVIKO-19 na wako kwenye hatari kubwa yakuwa na magonjwa sugu, wanaweza tumia dawa ya kunywa kama 'Paxlovid'. Dawa hiyo inatarajiwa kupunguza mahitaji yakulazwa hospitalini.
Msemaji wa chama cha Labor wa maswala ya uhamiaji na maswala ya nyumbani Kristina Keneally, amepatwa na UVIKO-19. Atajitenga kwa muda wa siku saba.
Shirika la Afya la Dunia (WHO) limeanza kufuatilia aina mpya ya kirusi cha Omicron. Imeongezea BA.4 na BA.5 kwenye orodha yake ya uchunguzi. WHO tayari inafuatilia BA.1 (aina halisi ya kirusi) na BA.2 (aina ya kirusi ambacho hakiko wazi), na BA.1.1 na BA.3.
Wasiwasi imeongezeka Marekani baada ya zaidi ya maafisi 50 wa serikali kupatwa na UVIKO-19, baada ya kuhudhuria tukio lajioni la mchezo wa Gridiron mjini Washington, DC mapema mwezi huu. Maafisa walio ambukizwa wanajumuisha wanachama wa ofisi za Rais na Naibu Rais.
Pata zahanati ya kupimia UVIKO-19
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya