Taarifa mpya ya UVIKO-19: QLD, ACT zapunguza hatua za afya wakati Australia inarekodi vifo 29

Hii ni taarifa yako mpya kuhusu UVIKO-19 nchini Australia kwa 5 Aprili.

People walk past a floral tribute to a delicatessen owner who died from Covid-19 in Melbourne last year. (file)

People walk past a floral tribute to a delicatessen owner who died from Covid-19 in Melbourne last year. (file) Source: Getty Images/WILLIAM WEST/AFP

Jumanne, Australia iliripoti vifo 29 vya UVIKO-19, 12 vikiwa New South Wales na nane katika jimbo la Victoria nane jimboni Queensland na kifo kimoja kiliripotiwa Australia Capital Territory (ACT). 

Mamlaka wa The ACT wameregeza zaidi  kuanzia saa tano dakika hamsini na tisa Jumatatu, 4 April 2022. 

Wasafiri wakimataifa ambao wamechanjwa hawatakiwi tena kufanya kipimo cha UVIKO-19 ndani ya masaa 24 yakuwasili ACT, kama vipimo vyao vilirejesha matokoe chanya ya coronavirus wiki 13 kabla ya safari yao. Kabla muda huo ulikuwa wiki tisa.

Wasafiri ambao hawaja chanjwa wenye miaka 12 na miezi mbili hadi miaka 17, hawatakiwi tena kufahamisha idara ya Afya ya ACT wanapo wasili pamoja nakufanya karantini kwa siku saba.

Waziri wa Afya Greg Hunt ame hamasisha wa Australia wanao stahiki wachukue dozi zao za nne za chanjo. Amesema wakaaji wanao stahiki wanaweza changia chanjo zao za mafua pamoja na dozi yao ya pili ya jeki.

Watu wa Queensland wame alikwa washiriki katika utafiti wa usalama na ufanisi wa UVIKO-19 jimboni kote. Lengo la utafiti huo nikuelewa madhara ya UVIKO-19 na chanjo jimboni Queensland kwa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu.

 kupunguzwa jimboni kuanzia saa saba usiku wa Alhamisi, 14 Aprili 2022. 

Magharibi Australia (WA) kuruhusu kurejea kwa muda kwa safari za bahari chini ya masharti makali kuanzia 17 Aprili. Mwanzoni, meli ndogo zinazo safiri kati ya majimbo za abiria 350, zitaruhusiwa jimboni humo.

Wazazi wataruhusiwa tena katika sehemu za shule, kuwashusha nakuwachukua watoto wao, kufanya mikutano ya ana kwa ana na walimu, na mikutano ya mwaka wa shule kwa mhula wa 2 katika  hilo.

Wakaazi wa Kusini Australia  kwa siku saba kama mtu yeyote katika familia yake anapatwa na UVIKO-19. Wakaaji wa nyumba hiyo lazima wafanye vipimo vya PCR katika siku ya sita au matokeo ya kipimo cha rapid antigen test katika siku za 1, 3, 5 na 7 (baada ya kila siku moja) kama hakuna dalili za UVIKO-19.                                        

Serikali ya NSW kutoka uwekezaji wa $5 milioni kwa matukio yanayo lenga ustawi wa jamii na, kama sehemu ya mpango wao kupona kutoka janga la UVIKO-19.

Kiongozi wa Victoria, Daniel Andrews amerejea kazini baada yakukamilisha siku saba zakujitenga. Bw Andrews alipatwa na UVIKO-19 28 March.  


Takwimu za UVIKO-19 Australia kwa 5 Aprili 2022

New South Wales: kesi mpya 19,183 zimerekodiwa, watu 1,467 wamo hospitalini, 56 wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na vifo 12 vimerekodiwa 

Victoria: kesi mpya 12,007 zimerekodiwa, watu 329 wamo hospitalini, 18 wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na vifo nane vimerekodiwa 

Tasmania: kesi mpya 2,437 zimerekodiwa, watu 44 wamo hospitalini, wawili wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na jimbo hilo halija rekodi vifo vyovyote. 

Queensland: kesi mpya 9,946 zimerekodiwa, watu 479 wamo hospitalini, 15 wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na vifo nane vimerekodiwa 

Australian Capital Territory: kesi mpya 918 zimerekodiwa, watu 418 wamo hospitalini, tano wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na kifo kimoja kilirekodiwa 

Magharibi Australia: Kesi mpya 8,145 zimerekodiwa, watu 242 wamo hospitalini, sita wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na vifo tano vyakihistoria kuanzia 31 Machi vimerekodiwa.

 


 


 



Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19 hapa



Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya 



Kama unahitaji msaada wa fedha, 

Hapa kuna msaada waku saidia kuelewa 



Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika Kiswahili kwenye.  


Share
Published 5 April 2022 4:48pm
Presented by Gode Migerano


Share this with family and friends