- Jimboni NSW, 59.25% ya umma unao stahiki ume pata chanjo kamili.
- Jimboni Victoria, Geelong na Surf Coast kuondoka katika amri yakubaki ndani kuanzia usiku wa manane.
- ACT yarekodi kesi mpya 25 ndani ya jamii.
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 961 ndani ya jamii pamoja na vifo tisa.
Dr Jeremy McAnulty kutoka idara ya afya ya NSW amesema idadi kubwa ya takwimu hizo zilikuwa katika vitongoji vya wasiwasi vinavyo jumuisha vitongoji vya; Guildford, Auburn, Punchbowl, Penrith, Bankstown, Liverpool na Bossley Park.
Kiongozi wa jimbo hilo Gladys Berejiklian amesema taarifa kuhusu jinsi jimbo hilo, lita safiri katika mchakato wakupona kutoka COVID unakamilishwa, na utatolewa wiki ijayo. Mamlaka wanapanga kutangaza baadae, hatua za afya kwa sehemu ya umma ambayo haija chanjwa.
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 779 ndani ya jamii pamoja na vifo viwili.
Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema baadhi ya vizuizi vita regezwa katika maeneo ya kanda ya Victoria na maeneo ya Jiji la Melbourne jimbo hilo litakapo fika kiwango cha 80% ya watu ambao wame pokea dozi ya kwanza ya chanjo ya COVID, hatua ambayo inatarajiwa kufanyika Jumanne, 28 Septemba.
Umbali wakusafiri kutoka nyumbani kwa watu kuta ongezwa hadi 15 km na ruhusa ita tolewa kwa mazoezi ya nje, kucheza gofu, tennis pamoja na mpira wa vikapu, kwa vikomo vya idadi ya watu. Vizuizi vitaregezwa pia kwa wanao ongozwa na mwalimu kufanya mazoezi kwa watu ambao wamepata chanjo kamili.
Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- Katika wilaya ya ACT, asilimia 85 ya umma wenye zaidi ya miaka 12 wamepokea dozi yao ya kwanza ya chanjo ya COVID-19.
- Queensland haija rekodi kesi yoyote mpya ndani ya jamii.
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: