- Jimboni New South Wales, wauguzi wana andamana kuomba ongezeko la wafanyakazi wakuwahudumia wagonjwa, pamoja na nyongeza kwa mishahara yao. Hatua hiyo ili anza saa moja asubuhi na itadumu kwa muda wa msaa 24.
- Maandamano hayo yanafanyika mjini Sydney, mbele ya bunge la NSW.
- Waziri wa Afya wa NSW alisema uamuzi wa chama cha wafanyakazi kuendelea mbele na maandamano hayo, ni "tendo lakusikitisha", baada ya Tume ya maswala yakazi kuamuru maandamano hayo yasifanywe.
- Wakati wa maandamano hayo, huduma zakuokoa maisha, zitaendelea katika hospitali zote za umma pamoja nakatika huduma za afya.
- Chanjo ya Novavax inayo tengezwa kupitia proteini, kwa sasa imo ndani ya zahanati zama GP, maduka yamadawa na katika vituo vya chanjo vinavyo simamiwa na serikali ya jimbo.
- Chanjo hiyo ime idhinishwa kwa matumizi katika watu wenye zaidi ya miaka 18 kwa dozi zao za kwanza naza pili. Chanjo hiyo kwa sasa haitolewi kwa watu wenye chini ya miaka 18 pamoja na kama chanjo za jeki.
- Waziri wa Afya wa Shirikisho Greg Hunt anatumai chanjo hiyo itatoa "chaguzi mpya" kwa wale ambao "wame subiri au hawakuweza chukua chanjo zingine zilizo kuwepo.".
- Tovuti ya kwa sasa inatoa fursa zakutafuta upatikanaji wa chanjo ya Novavax kote nchini Australia.
- Kiongozi wa Upinzani wa Victoria Matthew Guy ametozwa faini ya $100, kwa kutovaa barakoa ndani ya bunge la jimbo hilo. Wabunge wengine wanne wa Victoria nao pia wame pewa faini.
- Idadi ya wagonjwa wa UVIKO-19 walio lazwa katika hospitali za Victoria, ni ndogo zaidi tangu mwanzo wa mwaka.
- Jeshi la Ulinzi la Australia lita saidia kutoa huduma ndani ya vifaa vitatu vya huduma yawazee jimboni Tasmania, ambavyo vime kumbwa na mlipuko wa UVIKO-19, Naibu Kiongozi wa jimbo hilo na Waziri wa Afya Jeremy Rockliff amesema.
Takwimu za UVIKO-19
Jimbo la New South Wales liliripoti idadi ya wagonjwa 1,583 walio lazwa hospitalini, 96 kati yao wakiwa ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti. Kume ripotiwa pia vifo 16, pamoja na kesi mpya za maambukizi 8,201 za UVIKO-19.
Jimboni Victoria, watu 441 wame lazwa hospitalini, 67 kati yao wakiwa ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na 14 wanapumua kwa msaada wa mashine. Kuliripotiwa vifo 20 pamoja na maambukizi mapya 8,162 ya virusi.
Jimboni Queensland, kulikuwa kesi mpya 5,286 za UVIKO-19 pamoja na vifo 10. Wagonjwa 462 wame lazwa hospitalini, 35 kati yao wakiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti na 16 kati yao wanapumua kwa msaada wa mashine.
Jimbo la Tasmania halijarekodi vifo vyoyvote, ila kuna kesi mpya 513 za UVIKO-19. Watu 10 wamelazwa hospitalini wakitibiwa UVIKO-19, na mmoja wao yumo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti.
Na katika jimbo la Kusini Australia kuna kesi mpya 1,138 za UVIKO-19 ambazo zimeripotiwa, watu 219 wame lazwa hospitalini, 18 kati yao wana hudumiwa ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na 5 kati yao wanapumua kwa msaada wa mashine.
Majimbo kadhaa yana fomu zaku sajili matokeo ya vipimo vya RAT.
Karantini na vizuizi jimbo kwa jimbo
Safari
Msaada wakifedha
Kuna mageuzi kwa malipo ya janga ya UVIKO-19, punde majimbo yanapo fikia viwango vya 70% na 80% ya watu ambao wame pata chanjo kamili:
- Pata hapa Habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo mhimu kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .