Taarifa mpya kuhusu COVID-19: Mamlaka jimboni NSW na Queensland wahamasisha watu wabaki nyumbani

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia ya 3 August 2021.

Zahanati ya chanjo ya AstraZeneca katika kitongoji cha Wattle Grove

Zahanati ya chanjo ya AstraZeneca bila miadi katika kitongoji cha Wattle Grove, NSW Source: AAP Image/Joel Carrett

  • NSW yalenga kutoa dozi milioni 6 za chanjo kufikia mwisho wa Agosti.
  • Idadi ya wanao ugua jimboni Queensland yaongezeka hadi watu 47.
  • Victoria yarekodi kesi nne mpya.
  • Serikali ya shirikisho yatoa msaada wa ziada wa malipo ya COVID.

New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 199 ndani ya jamii, na angalau kesi 50 ndani ya jamii zilikuwa katika hali ambukizi.

Afisa Mkuu wa Afya Dr Kerry Chant amewakumbusha watu wasitembelee  isipokuwa kama ni lazima.   

Naye kiongozi wa jimbo hilo Gladys Berejiklian anataka jimbo lake lirekodi chanjo milioni sita kufikia mwisho wa Agosti. Kufikia sasa, idadi ya chanjo milioni 3.9 zimetolewa. 

Queensland
Queensland imerekodi kesi mpya 16 ndani ya jamii, zote ziki ungwa na mlipuko wa sasa.

Afisa Mkuu wa Afya Dr Jeannette Young amewahamasisha wakaaji kutoka  wabaki nyumbani na wapimwe punde wanapo hisi dalili zozote.

Naibu Kamishna wa Polisi Steve Gollschewski amesema kufikia sasa jeshi la polisi limetoa hati za adhabu 70 pamoja nakuwakamata watu 21, ambao hawaku fuatilia amri za afya ya umma.

Hali ilivyo kuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
  • Victoria imerekodi kesi nne mpya ndani ya jamii, zote zikiungwa na milipuko ya sasa na zilikuwa ndani ya karantini wakati zilikuwa katika hali ambukizi.

  • Watu ambao wamepoteza angalau masaa 8 ya kazi kwa sababu amri za afya ya umma jimboni humo, wanastahiki kupokea  kwa nyongeza ya malipo yao ya kawaida. Madai ya msaada huo wa ziada yame anza kupokewa leo.

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti ya vipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na mikoa:


ACT  na 
NT  na 
QLD  na 
SA  na 
TAS  na 
WA  na 
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni.  kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .





Pata rasilimali zilizo tafsiriwa na huduma yamawasiliano ya kitengo cha afya cha tamaduni mbali mbali cha NSW hapa:


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na mkoa:


 
 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo na mkoa:

 
 

Share
Published 3 August 2021 2:20pm
By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends