- Victoria yatangaza mfuko wa $21milioni kupiga jeki viwango vya chanjo
- Ongezeko ya kesi katika kanda ya NSW yazua wasiwasi
- ACT yatangaza uamuzi wakuregeza vizuizi
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 1,749 za maambukizi ya COVID-19 na vifo 11.
89.4% ya umma wenye zaidi ya miaka 16 jimboni humo wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo, na 67.2% wamepokea dozi zote mbili.
Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews ametangaza mfuko wa uwekezaji wa $21 milioni kupiga jeki chanjo, kujumuisha zahanati za ziada za chanjo, kuomba miadi ya, usafiri na mbinu mbadala zinapo hitajika katika jamii.
Serikali ya Victoria imethibitisha itaongeza muda mfupi wakujitenga, kwa orodha yake ya mageuzi ya sheria, jimbo hilo litakapo fikisha kiwango cha 70% ya lengo ya watu ambao wamepata chanjo mbili.
New South Wales
New South Wales imerekodi kesi mpya 273 za maambukizi ndani ya jamii pamoja na vifo vinne.
Chini ya 75% ya watoto wenye miaka kati ya 12-15 wamepokea dozi yao ya kwanza ya chanjo ya COVID-19, wakati 35.5% yao wamepokea chanjo kamili.
Jimbo hilo limepitisha pia lengo la 80% ya chanjo kamili kwa umma wenye zaidi ya miaka 16.
Afisa Mkuu wa Afya Dr Kerry Chant amesema ongezeko ya kesi za maambukizi katika maeneo ya kanda, inaendelea kuwa sehemu ya wasiwasi na jamii imehamasishwa ichanjwe.
ACT
ACT imerekodi kesi mpya 24, kesi 21 kati yazo zina ungwa na mlipuko wa sasa.
Wilaya hiyo imetangaza uamuzi wakuregeza vizuizi vya COVID-19, kama jibu kwa 80% ya chanjo kamili ya umma wenye miaka 12 na zaidi.
Biashara zote za rejareja, na biashara mhimu pamoja na zisizo mhimu, zitaruhusiwa kufunguliwa kuanzia saa 5:59 usiku wa Alhamisi 21 Oktoba.
Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- Queensland imeweka wazi kwa usafiri wa ndani nakimataifa, jimbo hilo litakapo fikisha kiwango cha 70%, 80% na kisha 90% ya umma unao stahiki ambao umepata chanjo kamili.
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: