Taarifa mpya ya COVID-19: NSW yaongeza orodha yawafanyakazi mhimu wakati maeneo ya maambukizi yaongezeka Victoria

Taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia 18 Julai 2021.

Sehemu ya nje ya jengo la Isola katika kitongoji cha Richmond, Melbourne, Sunday, July 18, 2021.

Mamlaka wa afya wa Victoria wamefunga jengo la Isola katika kitongoji cha Richmond, baada ya mkaaji kupatwa na Covid-19. Source: (AAP Image/James Ross)

  • NSW ime ongeza orodha yake ya wafanyakazi wanao ruhusiwa kuondoka Fairfield, Canterbury-Bankstown na Liverpool
  • Idadi ya sehemu za maambukizi ya COVID-19 Victoria inaendelea kuongezeka.
New South Wales
New South Wales imerekodi kesi mpya 105 za coronavirus ndani ya jamii. Kesi 66 zime ungwa na mlipuko usio julikana; chanzo cha kesi 39 bado ina chunguzwa. Mwanamke mwenye umri wa miaka 90 amefariki katika eneo la Kusini Mashariki Sydney. 

Wakaaji katika vitongoji vya  na  hawa ruhusiwi kuondoka katika vitongoji hivyo isipokuwa kama wanafanya kazi katika sekta ya huduma ya afya, huduma za dharura au ndani ya masoko, duka zinazo uza pombe, duka za bidhaa za rejareja, ofisi, duka zinazo uza bidhaa za wanyama pamoja na vituo vya shamba.

Kuanzia 12:01 ya asubuhi ya Jumatatu 19 Julai, kazi zote za ujenzi na kazi zote zo ukaribati ambazo si za haraka, pamoja na huduma za usafi na kazi za ukarabati kwa makazi ya watu zita sitishwa. Inatarajiwa vizuizi hivi vita waathiri wafanyakazi wa ujenzi takriban laki tano jimboni NSW.

Pata hapa,  kwenye orodha au ramani. Makatazo ya sasa yata ongezwa hadi saa 11:59 usiku wa Ijumaa tarehe 30 Julai 2021.

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 16 za coronavirus ndani ya jamii, na kesi 2 zilipatikana kutoka ng'ambo. Idadi kamili ya kesi jimboni VIctoria ni 70.

Kuna zaidi ya sehemu mpya 215 za maambukizi. Sehemu mpya za hivi karibuni ni Altona Meadows, Kew na vitongoji vya Truganina. Wakaaji wa Philip Island Kusini Mashariki ya Melbourne wame hamasishwa pia wapimwe. Pata hapa katika orodha au ramani. Makatazo ya tano yanatarajiwa kudumu hadi saa 11:59 usiku wa Jumanne, 20 Julai 2021.  

Masaa 24 yaliyo pita nchini Australia

  • ACT na Queensland zimerekodi siku nyingine yakutokuwa na maambukizi yoyote ndani ya jamii. 

  • Kusini Australia takriban dozi 100,000 za chanjo, zimetolewa katika eneo la maonesho la Adelaide katika kitongoji cha Wayville.

  • Tasmania yafunga mipaka na yote na NSW.
Sherehe ya Eid al Adha (“Sherehe ya kafara”) inaanza jumatatu, 19 July 2021. Ni muhimu kujilinda na wengine wakati wa sala za Eid al-Fitr kwaku: 

  • chagua kuombea nyumbani 
  • kufuta mikusanyiko mikubwa
  • kuvaa barakoa yako
  • kutumia mkeka wako binafsi wa sala
Hadithi potovu za COVID-19:
Vijana wenye afya nzuri hawa aathiriwi na COVID-19. Ina wadhuru zaidi na kuwauwa wazee au wagonjwa.

UKWELI wa COVID-19:
Virusi vina waathiri wazee nawatu wenye magonjwa sugu ila, huathiri na kuuwa baadhiya vijana wenye afya nzuri. 


Karantini, usafiri, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Masharti ya karantini na vipimo, yana simamiwa nakutekelezwa na serikali za majimbo na mikoa:


ACT  na i
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba ruhusa mtandaoni.  kwa taarifa kuhusu masharti yakuondoka Australia. 

 

Kuna hatua za muda kwa safari za ndege zakimataifa, ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, na taarifa hiyo huchapishwa kwenye tovuti ya .




Tembelea shirika la NSW Multicultural Health Communication Service:

Zahanati za vipimo katika kila jimbo na mkoa:


 
 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo na mkoa:

 
 

Share
Published 18 July 2021 5:28pm
By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends