- Watu milioni tano wamepokea dozi yao ya kwanza NSW
- Miada ya ziada ya chanjo, ipo Victoria
- Kesi mbili mpya zapatikana ndani ya jamii ACT, na sufuri kwa QLD
- Dozi milioni moja za ziada za Pfizer, zatarajiwa kuwasili nchini Australia leo usiku.
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 415 ndani ya jamii na vifo vinne. Kesi 35 zilikuwa ndani ya jamii wakati zilikuwa katika hali ambukizi.
Baadhi ya vitongoji ambavyo vina idadi nyingi ya kesi ni: Blacktown, Mount Druitt, Merion, Maryland, Auburn na Guildford.
Kiongzo wa jimbo hilo, Gladys Berejiklian amesema serikali inatafuta "fursa" kwa watu ambao wame chanjwa, wapate uhuru kuanzia September, jimbo hilo likiwa limerekodi idadi ya 50% ya watu wazima katika umma ambao wame pokea sehemu ya chanjo.
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 25 ndani ya jamii, kesi 4 miongoni mwa hizo hazija unga kwa milipuko inayo julikana. Kesi 13 zilikuwa ndani ya jamii wakati zilikuwa katika hali ambukizi.
Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews, amesema miadi elfu 84,000 itatolewa leo kwenye tovuti ya serikali.
Hali ilivyo kuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- Queensland haija rekodi kesi yoyote ndani ya jamii na, imetuma polisi wa ziada katika mpaka wake na NSW.
- ACT imerekodi kesi mbili mpya ndani ya jamii, moja yazo chanzo chake ikiwa haijulikani.
- Serikali ya madola imepata dozi milioni moja za chanjo ya COVID-19 ya Pfizer, hiyo ikiwa ni kwa nyongeza ya chanjo milioni 40 ambazo Australia ilikuwa inatarajia kupokea tayari.
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti ya vipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali za majimbo na mikoa:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa ya ziada kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua zamuda kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa na serikali nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata taarifa na habari katika zaidi ya lugha 60 kwenye tovuti hii:
- Pata miongozo inayo faa kwa jimbo na wilaya yako hapa: , , , , , , .
- Information about the .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa na huduma yamawasiliano ya Afya ya tamaduni mbali mbali ya NSW:
Pata hapa taarifa kuhusu zahanati za chanjo, katika kila jimbo na wilaya:
Pata hapa taarifa kuhusu malipo ya janga, katika kila jimbo na wilaya: