Miji ya Byron, Kempsey na Tweed jimboni NSW yarejea tena katika amri yakuto toka nje
- Victoria kwa sasa ina kesi 6,000 za COVID-19
- ACT yatangaza uwekezaji wa ziada kwa huduma za afya ya akili
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 1,022 ndani ya jamii pamoja na vifo 10. Kwa sasa, 53% ya wakaaji wanao stahiki jimboni humo wame pata chanjo kamili.
Miji ya Byron Shire, Kempsey na halmashauri ya jiji ya Tweed zita ingia katika amri yakuto toka ndani kwa muda wa siku saba kuanzia saa kumi na moja jioni ya leo, baada ya kesi chanya ya COVID kutoka Sydney kutembelea jamii kadhaa za pwani ya kaskazini ya NSW.
Kuanzia leo, kundi la watu watatu wenye chini ya miaka 18 wana weza tembeleana nyumbani mwao kama, wanaishi katika eneo la mzunguko wa kilomita tano au katika kitongoji kimoja. Ruhusa hiyo yamarafiki kutembeleana, imetolewa tu kwa nyumba ambako watu wazima wote wame pokea chanjo kamili.
Shirika la Msalaba Mwekundi la Australia linatoa kwa watu ambao wana viza za muda mfupi au watu ambao hawana viza na wame athiriwa kwa amri zakuto toka nje jimboni NSW.
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 603 ndani ya jamii pamoja na kifo kimoja.
Katika maeneo ya jiji la Melbourne, Geelong, Surf Coast, Ballarat na Mitchell Shire, sekta ya ujenzi imefungwa kwa muda wa wiki mbili baada ya milipuko kadhaa ya maambukizi iliyo ungwa na sekta hiyo ya ujenzi.
Kwa sasa kuna idadi ya kesi chanya 403 za maambukizi, ambazo zina ungwa na sekta hiyo, na pia zina husiana na maeneo 186 ya ujenzi.
Victoria inatarajia kupokea zaidi ya chanjo laki tatu za Moderna zitakazo sambazwa kote jimboni humo.
Australian Capital Territory
Wilaya ya ACT imerekodi kesi mpya 16 ndani ya jamii.
Kiongozi wa ACT Andrew Barr ametangaza uwekezaji wa ziada wa dola milioni 14, kwa mashirika yanayo toa huduma za msaada wa afya ya akili, pombe pamoja na mihadarati ndani ya wilaya hiyo.

Domestic infographic Source: SBS
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: