- Kuanzia kesho baadhi ya vizuizi vitaregezwa jimboni NSW
- Jimboni Victoria, kuna miadi 7,000 ya dozi ya kwanza ya chanjo ya Pfizer
- ACT imerekodi kesi mpya 15 na Queensland haijawa na kesi yoyote mpya ndani ya jamii
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 1,262 ndani ya jamii, pamoja na vifo saba.
Kuanzia tarehe 13 Septemba, idadi ya wakaaji 5 ambao wame pokea chanjo kamili wanao ishi nje ya wataruhusiwa kukutana nje ya nyumba zao. Wanao ishi ndani ya halmashauri hizo za wasiwasi wanaweza enda nje kufanya mazoezi au katika bustani, pamoja na wanachama wa nyumba zao ambao wame pokea chanjo kamili, kwa muda wa masaa mawili kila siku kwa nyongeza ya muda wa mazoezi bila kikomo.
Kiongozi wa jimbo hilo Berejiklian amesema, jimbo hilo lina lengo lakufungua mipaka yakimataifa kufikia wakati wa krisamasi, wakati inatarajiwa 78% ya umma wenye zaidi ya miaka 16 watakuwa wame pokea dozi ya kwanza ya chanjo, na 45.58% ya umma itakuwa imepokea chanjo kamili.
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 392 mpya ndani ya jamii.
Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema kuna miadi 7,000 ya dozi za kwanza za Pfizer, katika wiki zijazo ndani ya zahanati zinazo simamiwa na serikali ya jimbo hilo.
Vituo vipya vya chanjo vitafunguliwa kote jimboni Victoria ndani ya shule nane na katika halmashauri za jiji za; Hume, Dandenong na Casey, kanisa la Greek Orthodox Church katika kitongoji cha Thornbury, hekalu laki Hindu katika kitongoji cha Mill Park pamoja na katika msikiti ambao uko katika kitongoji cha Newport.
Hali ilivyo kuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- Waziri Mkuu Scott Morrison ametangaza uwepo wa dozi milioni za ziada za, chanjo ya COVID-19 za Moderna, ambazo zime pendekezwa kwa kila mtu mwenye zaidi ya miaka 12.

Source: ALC
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: