- NSW yarekodi kesi mpya 830 za COVID-19 na vifo vitatu
- Kesi mpya 65 za COVID-19 zarekodiwa Victoria, kesi 21 zime unga na mlipuko wa Shepparton
- ACT yarekodi kesi mpya 19 za coronavirus
- Queensland haija rekodi kesi yoyote ya COVID-19 katika masaa 24 yaliyo pita
New South Wales
NSW yaweka rekodi nyingine yakila siku ya kesi mpya 830 za COVID-19.
NSW ilirekodi pia vifo vitatu ambavyo viliwahusu wanaume wawili, mmoja akiwa na miaka 60 na mwingine 70 wawili hao wakiwa walikuwa wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo ya COVID-19, pamoja na mwanamke mwenye miaka 80 ambaye alikuwa haja chanjwa na alikuwa mtu wakaribu wa aliyekuwa na virusi hivyo. Kupitia vifo hivyo vitatu, idadi kamili ya vifo kupitia mlipuko wa sasa imefika 71.
Kwa sasa kuna watu 550 hospitalini ambao wanapokea matibabu ya COVID-19, watu 94 kati yao wakiwa katika hali mahtuti.
Waziri wa Afya Brad Hazzard amesema NSW imerekodi viwango "visivyo vya kawaida" vya chanjo katika siku chache zilizo pita.
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 65 za COVID-19, kesi 55 ziki ungwa na milipuko ya sasa na kesi 10 zina fanyiwa uchunguzi.
Ni kesi 12 tu ambazo zilikuwa zinajitenga kwa muda wato ambao zilikuwa katika hali ambukizi.
Katika kesi zilizo sajiliwa leo, angalau 21 zili ungwa na mlipuko katika mji wa kanda wa Shepparton.
Wakaaji wa Victoria waliamka leo asubuhi nakupata, jimbo zima likiwa chini ya vizuizi.
Jeshi la Polisi la Victoria limeripoti zaidi ya watu 200 wamekamatwa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa katika maandamano dhidi ya kufungiwa ndani mjini Melbourne jana.
Hali ilivyokuwa katika masaa 24 nchini Australia
- ACT imerekodi kesi mpya 19 za COVID-19, kesi sita zilikuwa ndani ya jamii wakati zilikuwa katika hali ambukizi. Mwanafunzi wa chuo cha ANU alipatwa na virusi hivyo ila alikuwa akijitenga.
- Queensland imekuwa na siku nyingine ambayo haija rekodi kesi yoyote, wakati kuna kesi 39 zinazo tibiwa.

Source: ALC
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti ya vipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa ya ziada kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa, ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali na huchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60 kwenye tovuti hii
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo na wilaya yako: , , , , , , .
- Pata taarifa hapa kuhusu .
Pata hapa rasilimali zilizo tafsiriwa nakuchapishwa na huduma yamawasiliano ya afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika lika jimbo na wilaya: