- Mzigo wa kwanza wenye chanjo ya Novavax umewasili Australia kutoka Singapore. Mzigo huo una dozi za kwanza milioni tatu ambazo zita tolewa kote nchini 21 Februari.
- Idadi ya maafisa 1,700 wa jeshi la ulinzi la Australia, wata tumwa kupunguza shinikizo kwa mfumo wa huduma ya wazee hata hivyo, watetezi wanasema haitoshi tu kupunguza uhaba wa wafanyakazi.
- Jimboni NSW, 44% ya umma unao fuzu kwa sasa wame pata dozi yao ya tatu ya chanjo ya UVIKO. Jimboni Victoria 46% ya watu wazima wame pokea dozi zao za tatu.
- Serikali ya Victoria ita tanua upatikanaji wa vifaa vya vipimo vya rapid antigen, kama familia za watoto wenye miaka mitatu hadi tano wanao pokea huduma ya watoto, wata peleka vipimo hivyo nyumbani katika wiki zijazo.
- Wakati idadi ya kesi za maambukizi zinaendelea kupungua katika majimbo mengi, Wilaya ya Kaskazini ina kiwango cha juu nchini Australia cha watu walio lazwa hospitalini kwa sababu ya hali zinazo husiana na UVIKO.
Takwimu za UVIKO-19:
NSW imeripoti idadi ya wagonjwa 2068 wamelazwa hospitalini, wagonjwa 132 kati yao wakiwa ndani ya kitengo cha hali mahtuti. Kuna vifo vipya 18 na, kesi mpya 9,690 za maambukizi ya UVIKO-19.
Jimboni Victoria, watu 575 wame lazwa hospitalini, watu 72 wako ndani ya kitengo cha hali mahtuti. Kume ripotiwa vifo 20 pamoja na maambukizi mapya 9,785.
Jimboni Queensland watu 705 wame lazwa hospitalini, idadi hiyo inajumuisha watu 45 ambao wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti, vifo 12 vimeripotiwa pamoja na kesi mpya 5,178 za maambukizi.
Nalo jimbo la Tasmania lina watu 15 ambao wame lazwa hospitalini, kuna kesi mpya 601 za maambukizi na jimbo hilo halija ripoti vifo vyovyote.
Majimbo kadhaa yana fomu zaku sajili matokeo ya vipimo vya RAT.
Karantini na vizuizi jimbo kwa jimbo
Safari
Msaada wakifedha
Kuna mageuzi kwa malipo ya janga ya UVIKO-19, punde majimbo yanapo fikia viwango vya 70% na 80% ya watu ambao wame pata chanjo kamili:
- Pata hapa Habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo mhimu kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .