- Waasafiri kutoka Australia ambao wame pata chanjo kamili wanao safiri kwenda New Zealand, hawata takiwa kujitenga tena kuanzia saa tano hamsini na tisa usiku wa Jumatano Machi 2.
- Sharti la kufanyiwa vipimo unapo wasili na baada ya siku ya 5 au 6 bado litasalia.
- Ni , wanajumuisha wakaaji wa nchi hiyo, wachumba wao, watoto wao na wazazi.
- Magharibi Australia itawasilisha vizuizi vikali kuanzia Alhamisi 3 Machi, siku ambayo jimbo hilo lita fungua mipaka yake.
- vitajumuisha amri zakuvaa barakoa kwa watoto kuanzia darasa la 3, watu 10 tu kuruhusiwa katika mikusanyiko ya watu nyumbani, matukio ya nje kuhudhuriwa na watu 500 tu na vyumba vya sanaa na filamu kuhudumia 50% ya wateja tu.
- Mamlaka wa Hong Kong wahajatupilia mbali uwezekano wa makatazo mapya yakutoka nje. Jana walirekodi kesi mpya za maambukizi 34,466, hali inaendelea kuwa ngumu wakati vifaa vya kuhifadhi maiti hospitalini na katika vyumba vya kuhifadhi maiti vya umma, vimefikia uwezo wao kamili.
Takwimu za UVIKO-19 Australia
New South Wales inawagonjwa 1,098 ambao wamelazwa hospitalini, 49 kati yao wakiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti. Kume vifo 9 jimboni humo na maambukizi mapya 8,874 ya UVIKO-19.
Jimboni Victoria, watu 255 wamo hospitalini na 41 kati yao wakiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti na watu 5 wanapokea msaada wa mashine kupumua. Kumeripotiwa vifo 18 pamoja na maambukizi mapya 6,879 ya virusi.
Tasmania haija rekodi vifo vyovyote ila kuna maambukizi mapya 957 ya UVIKO-19. Watu 13 wame lazwa hospitalini ambako wanatibia UVIKO-19, na watu wawili kati yao wanahudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti.
Katika wilaya ya ACT watu 45 wamelazwa hospitalini wakiwa na UVIKO-19, hakuka yoyote kati yao anaye hitaji huduma katika kitengo cha wagonjwa mahtuti, na wilaya hiyo imerekodi maambukizi mapya 692 ya virusi.
Jimboni Queensland, kume rekodiwa kesi mpya 4,453 za UVIKO-19 pamoja na vifo 10, Watu 316 wamelazwa hospitalini wakiwa na UVIKO-19, na wagonjwa 26 wanahudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti.
Katika jimbo la Kusini Australia watu 111 wame lazwa hospitalini wakiwa na UVIKO-19 na watu 9 kati yao wanahudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti, watu 2 kati yao wanapumua kwa msaada wa mashine. Kumeripotiwa vifo 2 pamoja na kesi mpya 1,618 za maambukizi.
Katika Wilaya ya Kaskazini kumeripotiwa kesi mpya 565 za UVIKO-19. Watu 86 kwa sasa wamelazwa hospitalini na wagonjwa 4 wanahudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti.
Katika jimbo la Magharibi Australia kulikuwa kesi mpya 1,179 za UVIKO-19 wakati watu 16 wamelazwa hospitalini, na hakuna yeyote kati yao anaye hitaji huduma ya wagonjwa mahtuti.
Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19 hapo chini
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa chini, kama matokoe ya kipimo chako ni chanya