- Kiongozi wa NSW asema ukosefu wa utiifu, unaongeza idadi ya kesi jimboni
- Wakaaji wa Victoria wapokea chanjo kwa wingi
- Kesi mpya za Queensland zilikuwa katika karantini wakati zilikuwa katika hali ambukizi
- Utawala wa Bidhaa na Tiba umetoa chanjo ya COVID-19 ya Moderna idhini ya muda
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 356 ndani ya jamii, theluthi tatu kati yao walikuwa katika hali ambukizi ndani ya jamii. Wazee watatu ambao walikuwa hawaja chanjwa wame fariki, nakuongeza idadi ya vifo kupitia COVID-19 kufika 32 wakati wa mlipuko wa sasa.
Maeneo ya Byron Shire, Richmond Valley, Lismore na halmashauri ya jiji la Ballina kwa sasa ziko chini ya makatazo hadi saa sita dakika moja usiku wa Jumanne 17 Agosti 2021.
Kiongozi wa jimbo la NSW Gladys Berejiklian amesema ukosefu wa utiifu wa amri za afya ya umma, inaendelea kuwa sababu kubwa ya virusi kusambaa na amehamasisha kila mtu achanjwe.
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 20 ndani ya jamii ambazo zina ungwa na milipuko inayo julikana, na ni kesi tano tu ambazo zilikuwa ndani ya karantini wakati zilikuwa katika hali ambukizi.
Waziri wa afya jimboni humo Martin Foley amesema, kuna idadi ya miadi za chanjo laki tatu elfu thelathini na tatu katika mwezi ujao.
Wakaaji wa Melbourne wanao elekea katika maeneo ya kanda, wanaweza pewa faini za takriban dola elfu tano, wakati idadi ya polisi 200 wametumwa kupiga doria katika barabara kuu naza vichochoro jimboni humo.
Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- Queensland imerekodi kesi mpya tatu ndani ya jamii. Pata hapa
- Serikali ya shirikisho imepata dozi milioni 25 za chanjo za COVID-19 za Moderna, dozi milioni 10 zikitarajiwa kuwasili kabla ya mwisho wa 2021.
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti ya vipimo yanasimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na mikoa:
Kama unataka safiri nga'mbo, unaweza wasilisha ombi lako mtandaoni kupewa ruhusa. kwa taarifa ya ziada kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hufanyiwa tathmini mara kwa mara, na serikali pamoja nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata taarifa na habari katika zaidi ya lugha 60 kwenye tovuti hii
- Pata miongozo inayo faa kwa jimbo na mkoa wako hapa: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Pata rasilmali zilizo tafsiriwa na huduma ya mawasiliano ya idara ya afya ya tamaduni nyingi jimboni NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na mkoa:
Taarifa ya malipo ya janga katika kila jimbo na mkoa: