- Mashindano ya kombe la Melbourne kuruhusu watazamaji 10,000, ambao wame pata chanjo kamili kama sehemu ya jaribio la Victoria
- NSW yafikia lengo la kiwango cha asilimia 90 cha dozi za kwanza za chanjo, wakati jimbo hilo linajiandaa kufunguliwa tena kesho
- Maafisa wa Afya katika majimbo matatu wako katika hali ya tahadhari baada ya mfanyakazi wa ndege kutoka Victoria, kusafiri katika ndege za Virgin
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 1,890 za maambukizi ya COVID-19 ndani ya jamii pamoja na vifo vitano. Miongoni mwa wagonjwa 602 ambao wamelazwa hospitalini kwa sasa, ni chini ya asilimia 7 kati yao ambao wame pata chanjo kamili. Juhudi za ufuatiliaji wa watu wakaribu wa walio ambukizwa zime punguzwa, kulenga kesi chanya pamoja na watu wakwanza walio kutana na aliye ambukizwa.
Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews ametangaza mfululizo wamatukio kama sehemu kubwa ya majaribio, kwa jinsi uchumi wa jimbo hilo uta simamiwa jimbo hilo litakapo fikisha 80% ya viwango vya chanjo.
Melbourne itakuwa mwenyeji wa tamasha ya mziki tarehe 30 Oktoba, ambapo maelfu yawatu wata shiriki.
Shindano la kombe la Melbourne litakuwa tarehe 2 Novemba, na watazamaji 10,000 ambao wame pata chanjo kamili wataruhusiwa kushiriki.
New South Wales
New South Wales imerekodi kesi mpya 477 za maambukizi ndani ya jamii pamoja na vifo sita.
Jimbo hilo lime fikisha malengo yake ya chanjo 90% za kwanza, kwa wakaaji wenye zaidi ya miaka 16.
72.8% ya wakaaji wenye zaidi ya miaka 16 kwa sasa wame pata chanjo kamili.
Mradi wa ufuatiliaji wa maji taki wa shirika la Afya la NSW, umetambua chembe chembe za coronavirus katika vitu waliyo kusanya kutoka eneo la Uralla ambalo liko katika kanda ya Hunter New England.
Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- Queensland haija rekodi kesi zozote za COVID-19.
- Wilaya ya ACT imerekodi kesi mpya 30, 16 kati yazo zikiwa zime ungwa na zinazo salia ziko chini ya uchunguzi.
- Maafisa wa Afya katika majimbo matatu wako katika hali ya tahadhari baada ya mfanyakazi wa ndege wa Victoria, kufanyakazi ndani ya ndege iliyo fanya safari ya kwenda nakurudi kati ya Melbourne na Adelaide, Sydney na Newcastle wakati alikuwa katika hali ambukizi kati ya tarehe 4 hadi 6 Oktoba.
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: