- NSW yafikia utoaji wa 40% ya dozi mbili za chanjo
- Victoria yatangaza msaada kwa jamii ambazo katika hali mbaya
- ACT yaripoti kesi mpya 15 ndani ya jamii
- Queensland yaripoti kesi moja mpya ndai ya jamii
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 1485 ndani ya jamii, na vifo vitatu. Kuna zaidi ya watu elfu moja ndani ya hosptiali, 175 wako ndani ya kitengo cha hali mahtuti, na 72 kati yao wanapokea msaada wa kupumua kwa mashine.
NSW kwa sasa imefikia 40% ya watu ambao wamepokea dozi mbili na 73% ya watu ambao wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo. Kiongozi wa jimbo hilo Gladys Berejiklian amesema, "bila shaka jimbo hilo halitakuwa na makatazo ya jimbo zima tena", wakati 80% ya chanjo itakuwa imetolewa ila, ameonya kuwa idadi ya kesi itaongezeka katika wiki mbili zijazo.
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 183 ndani ya jamii, kesi 101 zikiungwa na milipuko inayo julikana.
Waziri Luke Donnellan alitangaza ongezeko uwekezaji wa $27 milioni kwa kuendeleza kwa jamii ambazo ziko katika hali mbaya.
Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- ACT yarekodi kesi mpya 15, 13 kati yazo zikiungwa na mlipuko unao julikana. Kesi sita zilikuwa ndani ya karantini muda wote zilikuwa katika hali ambukizi.
- Kesi moja mpya imerekodiwa Queensland, ikimhusu mama ya mtoto aliye patwa na virusi jana.
- Serikali ya WA yataka angalau 80% ya wakaaji wa Magharibi Australia wanao stahiki wachanjwe kabla, serikali hiyo iweke tarehe yaku ondoa vizuizi vigumu vya mpaka.

Source: ALC
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: