- Profesa Peter Collignon kutoka chuo cha taifa cha Australia ameomba mageuzi yafanywe kwa mawasiliano kuhusu chanjo za jeki. "Kadiri unavyo zeeka, ndivyo unavyo pata faida zaidi", alisema, nakuongezea kuwa kwa watu wenye zaidi ya miaka 50, tunastahili lenga kuwa na viwango vya chanjo za jeki kwa kiwango sawia na dozi za kwanza naza pili.
- Akizungumza katika kongamano la Australian Financial Review Business Summit, Waziri Mkuu Scott Morrison alisema kuwa "sintofahamu ya UVIKO, kwa masikitiko, itaendelea kuwa nasi ila, hatustahili iruhusu itutishe au itushinde".
- Kauli hiyo ilijiri kwa kutarajia mkutano ujao wa baraza lakitaifa Ijumaa 11 Machi. Viongozi wa majimbo na wilaya watajadili chakufanya kwa maandalizi ya msimu wa majira ya baridi, ambao unaweza leta ongezeko la maambukizi ya UVIKO-19 na, wakati kuna uwezekano mafua yanaweza rejea baada ya miaka mbili ya kuwa na visa vichache.
- Malkia Elizabeth II amekutana na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau katika mkutano ambao ulikuwa wake wa kwanza, tangu alipo patwa na UVIKO-19 Februari 20.
- Utafiti wa hivi karibuni wa chuo cha Oxford, umechapishwa katika jarida la Asili, utafiti huo umetambua madhara makubwa ya UVIKO-19 kwa ubongo, moja yazo ikiwa ni kupungua nakupoteza kwa tishu za ubongo.
- , baada yamadereva kadhaa wamabasi wa Perth kupatwa na UVIKO-19 au, wanadhaniwa kuwa ni watu wa karibu wa walio patwa na virusi hivyo. Hakuna njia za usifiri zitakazo futwa ila, upatikanaji wa usafiri unaweza punguzwa.
Takwimu za UVIKO-19 Australia
New South Wales iliripoti kuwa ina wagonjwa 1,070 ambao wame lazwa hospitalini, 43 yao wakiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti. Kume kuwa vifo 5 na kesi mpya 13,018 za maambukizi ya UVIKO-19.
Jimboni Victoria, watu 203 wame lazwa hospitalini, 29 kati yao wakiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti na 4 wakipumua kwa msaada wa mashine. Kume kuwa vifo 6 na maambukizi mapya 7,043.
Tasmania haija rekodi vifo vyovyote ila kuna kesi mpya 1,051 za UVIKO-19. Kuna watu 14 ambao wanapokea matibabu ya UVIKO-19 hospitalini, na watu 4 wanahudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti.
Queensland imeripoti kesi mpya 4,397 za maambukizi ya UVIKO-19 pamoja na vifo 5. Watu 268 wame lazwa hospitalini wakiwa na UVIKO-19, na watu 20 wanahudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti.
Katika ACT watu 43 wako hospitalini wakiwa na UVIKO-19, watu 2 wanahudumiwa ndani ya katengo cha wagonjwa mahtuti, na mamlaka wamerekodi kesi 658 za maambukizi mapya.
Katika jimbo la Magharibi Australia kuna kesi mpya 2,847 za maambukizi ya UVIKO-19, na watu 48 kwa sasa wame lazwa hospitalini.
Na katika Wilaya ya Kaskazini, kuna kesi mpya 437 za maambukizi ya UVIKO-19 pamoja na kifo kimoja. Watu 45 kwa sasa wamelazwa hospitalini na mtu mmoja anahudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti.
Na katika Jimbo la Kusini Australia watu 97 wame lazwa hospitalini wakiwa na UVIKO-19, na watu 13 kati yao wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti, na watu 2 wanapumua kwa msaada wa mashine. Jimbo hilo limerekodi pia kesi mpya 2,089 za maambukizi ya UVIKO-19.
Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19 hapo chini
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa chini, kama matokoe ya kipimo chako ni chanya