Mchezaji wa cricket wa Australia Mitchell Marsh yuko hospitalini baada yakupatwa na COVID-19 India.
Marsh anacheza katika timu moja na muAustralia mwenza David Warner katika timu ya Delhi Capitals katika ligi kuu ya cricket ya India.
Delhi Capitals kupitia taarifa imesema wanachama wake kadhaa, wafanyakazi wakijumuishwa wamerejesha matokeo chanya ya vipimo. Wote hawana dalili za ugonjwa ila, hali zao zinafuatiliwa kwa karibu.
Biashara NSW na chama cha Biashara na Viwanda cha Victoria, vimeomba serikali husika ziondoe sharti la kujitenga kwa siku saba ambazo zipo kwa sasa, kwa watu ambao ni wakaribu wa mtu aliye ambukizwa COVID-19.
Vikundi vya biashara vime laumu masharti yakujitenga, kwa uhaba wa wafanyakazi.
Vituo vyakutoa taarifa za chanjo za UVIKO-19, vimefunguliwa ndani ya masoko makubwa na matukio katika majimbo ya New South Wales, Victoria na Queensland.
Wakaaji wanaweza pata taarifa nakuomba miadi ya chanjo zao, katika vituo vifuatavyo kuanzia 18 hadi 24 Aprili:
NSW – Penrith, Westfield Penrith
NSW – Campsie, Campsie SC
QLD – Broadbeach, Pacific Fair
QLD – Brown Plains, Grand Plaza
VIC – Dandenong, Dandenong Plaza
VIC – Narre, Warren Westfield Fountain Gate
Shirika linalo simamia maswala yakulinda umma dhidi ya hatari zakibaolojia na dharura kuhusiana na UVIKO-19 kwa Australia iliisha 17 Aprili. Inamaana kwamba wasafiri wanao ingia Australia, hawatakiwi tena kuwa na matokeo hasi ya kipimo cha UVIKO-19 kabla waje na meli za abiria zinaweza ingia Australia tena.
Kanuni za kuzuia kupandishwa kwa bei ya vipimo vya rapid antigen nazo zime isha.
Hata hivyo, wasafiri wakimataifa wanao ingia nakutoka Australia, bado wanatakiwa kutoa ushahidi wa chanjo zao mbili pamoja nakuvaa barakoa katika safari zakimataifa chini ya ushauri wamatibabu.
Wakaaji wa marekani hawatakiwi tena kuvaa barakoa ndani ya usafiri wa umma, baada ya mahakama yashirikisho kufuta sharti la miezi 14 lakuvaa barakoa jana Jumatatu.
Mji wa Shanghai umeripoti vifo vitatu vya UVIKO-19 kutoka mlipuko wa sasa ambao umetumbukiza mji huo mkubwa katika, makatazo yakutoka nje kwa muda wa wiki tatu. Hata hivyo, wasiwasi umezuliwa kuhusu usahihi wa takwimu hizo.
Pata zahanati ya kupimia UVIKO-19
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya