Jumanne, Australia iliripoti vifo 48 vya UVIKO-19, vifo18 vikiripotiwa Queensland, 16 Victoria na 14 New South Wales (NSW).
Kesi mpya za UVIKO-19 ziliongezeka kote nchini Australia baada ya kesi kupungua katika wikendi iliyopita na Jumatatu.
Idadi ya maambukizi ya kila siku Queensland yaliongezeka kutoka elfu 3,534 Jumatatu hadi 5,118 Jumanne. Nalo jimbo la Magharibi Australia liliripoti ongezeko ya kesi kutoka elfu 10,013 hadi elfu 12,114. Jimbo hilo liliripoti pia vifo sita vyakihistoria.0
Jimbo la Kusini Australia nalo liliripoti vifo 14 vyakihistoria, ambavyo vilirekodiwa kati ya 21 Machi 2022 na 22 Mei 2022.
Serikali ya Jimbo la Kusini Australia liliwashauri wazazi waripoti matokeo chanya ya vipimo vya RAT, vya watoto wao ndani ya masaa 24. Serikali ya jimbo imependekeza vipimo vya PCR kwa watoto ambao wana dalili za UVIKO-19 ila, matokeo yao ya vipimo vya RAT ni hasi.
Waziri wa Afya wa NSW Brad Hazzard, amesema hospitali za jimbo zinakabiliwa na tisho tatu za idadi kubwa ya kesi za UVIKO-19, ongezeko za kesi za mafua na wafanyakazi wanao chukua likizo bila malipo kwa sababu ya ugonjwa. Ame wahamasisha wakaazi wapate chanjo ya mafua bila kuchelewa.
Queensland ita anza kutoa chanjo za mafua bure kwa wakaazi wote wenye zaidi ya miaka sita kuanzia leo. Wakaazi wanaweza pata chanjo yao kupitia GP wao au duka lakuuza dawa hadi 30 Juni.
Mabanda yanayo toa taarifa ya UVIKO-19, yanatumika kwa sasa katika orodha ya masoko hapo chini hadi 29 Mei.
NSW - Tweed Heads - Tweed City Shopping Centre
NSW - Bankstown - Roselands Shopping Centre
QLD - Loganholme - Logan Hyperdome
QLD - Beenleigh - Beenleigh Marketplace
QLD - Southport - Australia Fair Shopping Centre
VIC - Cardinia - Pakenham Central
SA - Salisbury Downs - Hollywood Plaza
SA -Adelaide - Munno Para Shopping Centre
Pata zahanati ya kupimia UVIKO-19
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya