Australia iliripoti vifo 42 vya UVIKO-19, vifo 18 vikiwa New South Wales na vifo 15 Victoria, Jumanne. Takwimu kutoka Magharibi Australia zilijumuisha vifo saba vya kihistoria.
Abiria kumi na wafanyakazi wawili walipatwa na UVIKO-19 ndani ya meli yakitalii Magharibi Australia.
Meli hiyo yakitalii, Coral Discoverer, iliwasili mjini Broome mapema Jumatatu baada ya safari ya siku 10 Jumatatu kutoka Darwin. Abiria wote ndani ya meli hiyo wame pata chanjo tatu za UVIKO.
Magharibi Australia ilikuwa imeruhusu meli ndogo zakitalii, zenye abiria wasio zidi 350 na wafanyakazi, kuingia jimboni humo kuanzia 17 Aprili 2022.
Kuna uwezekano serikali ya Magharibi Australia inaweza futa amri zakuvaa barakoa wiki hii, wakati idadi ya kesi mpya za UVIKO-19 inaendelea kuto ongezeka jimboni humo.
Nancy Baxter, ni mtaalam masomo ya udhibiti wa magonjwa katika Chuo cha Melbourne, ana amini ni mapema sana kuregeza vizuizi wakati New South Wales, Victoria, Australian Capital Territory na Queensland wikijana zilitangaza hatua yakuondoa sheria yawatu wakaribu wa walio ambukizwa kujitenga pamoja na sheria za karantini.
"Sasa hivi, tuku katika hatua yaku kana ya janga, ambako tunataka ishi kama tulivyo fanya kabla," Profesa Baxter alieleza shirika la habari la Jumanne.
Beijing inafanya vipimo vya watu kwa wingi baada ya mlipuko mpya wa UVIKO-19. Jumatatu, afisa wa afya aliripoti maambukizi 70 katika vitongoji 16 vya mji huo mkuu wa taifa. Nyingi ya kesi hizo 46 zilikuwa katika kitongoji cha .
China imechukua hatua kali zaudhibiti wa usambaaji wa UVIKO-19, Mji wake mkuu wakibiashara Shanghai imekuwa chini ya amri yamakatazo yakutoka nje kwa muda wa wiki nne zilizo pita.
Pata zahanati ya kupimia UVIKO-19
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya