Jumanne, Australia iliripoti vifo 29 vya UVIKO-19, vifo 12 vikiwa Victoria, 8 New South Wales na 5 Kusini Australia. Jimbo la Magharibi Australia liliripoti vifo viwili vyakihistoria.
Kulinganisha na siku iliyopita, kulikuwa ongezeko katika idadi ya kesi mpya zilizo ripotiwa zakilasiku za UVIKO-19, pamoja na watu waliolazwa hospitalini katika majimbo mengi kote nchini Australia.
Jimbo la Victoria liliripoti idadi kubwa ya kesi za kilasiku Jumanne, hiyo ikiwa ni ongezeko kutoka 7,557 Jumatatu hadi 9,181. Queensland iliripoti ongezeko yakesi kutoka 2,548 hadi 4,288.
Tazama maendeleo ya UVIKO-19 kwa kesi mpya, idadi ya wanao lazwa hospitalini pamoja na vifo nchini Australia .
Kaimu Afisa Mkuu wa Afya Dkt Sonya Bennett, ana wahamasisha waaustralia wote wanao weza pata chanjo ya mafua wafanye hivyo. Serikali ya Australia, kupitia (NIP), inatoa chanjo yabure ya mafua kila msimu, kwa vikundi ambavyo viko hatarini kwa mafua. Vikundi hivyo vinajumuisha, waaustralia wakwanza, watoto wachanga, vijana, wanawake wajawazito pamoja na mtu yeyote mwenye zaidi ya miaka 65.
Tangu jana, the Australian Capital Territory inatoa chanjo za mafua bure kwa wamiliki wakadi zamisaada katika zahanati zake za chanjo. Miadi katika zahanati hizo ambazo ziko Weston, kwa wamiliki wa kadi hizo pamoja na watoto wao, inaweza fanywa kupitia simu kwa namba hii 02 5124 3999 kati ya saa 2 asubuhi na saa 11 jioni Jumatatu hadi Ijumaa.
Kuanzia 8 Juni 2022, wakaaji wa Canberra wenye miaka 5 na zaidi, wataweza pata chanjo zao za mafua kutoka maduka yanayo uza dawa. Kwa sasa maduka yanayo uza madawa, yanaweza toa chanjo tu kwa watu wenye miaka 10 na zaidi.
Wakaaji wote wenye umri wa miezi sita na zaidi jimboni New South Wales, Victoria, Queensland, Magharibi Australia, Kusini Australia na Tasmania wanastahiki kupokea chanjo bure za mafua katika mwezi wa Juni.
Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya