Jumanne, Australia iliripoti vifo 95 vya UVIKO-19, vifo 47 vikiwa New South Wales (NSW), 22 Queensland na 13 Victoria.
Australia inakaribia takwimu nyingine mbaya ya vifo 12,000 vya UVIKO-19, kume kuwa idadi ya vifo 11,959 tangu janga lilipo anza.
Maambukizi ya kila siku yame pungua katika baadhi yamajimbo katika siku chache zilizo pita, yaki onesha ishara za mapema kuwa maambukizi ya Omicron ya sasa yana fikia kilele katika maeneo husika.
Hata hivyo, idadi ya wanao lazwa hospitalini nakupokea huduma ya wagonjwa mahtuti inaendelea kuwa kubwa. Jumanne, NSW iliripoti kuwa watu 76 ambao wana UVIKO-19 wame lazwa ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti, takwimu kubwa zaidi ya jimbo hilo tangu Aprili.
Tazama maendeleo mapya ya UVIKO-19, kwa kesi mpya, idadi ya wanao lazwa hospitalini pamoja na vifo nchini Australia .
Kiongozi wa Queensland Annastacia Palaszczuk, akinukuu mfumo wakisayansi, amesema wimbi la tatu au la sasa la Omicron jimboni mwake, linaweza fikia kilele mwisho wa Agosti. Idadi ya wanao lazwa hospitalini imekuwa ikipungua katika siku chache zilizo pita.
Mamlaka wa Afya wa Victoria, wana amini jimbo hilo lime pita kilele chake wiki jana ila, wameonya kuwa huenda kulikuwa matukio yakuto toa ripoti kamili kuhusu maambukizi mapya ya UVIKO-19.
Australia ilisitisha Oparesheni ya Kinga ya UVIKO 1 Agosti. Ilizinguliwa Juni mwaka jana, kuhakikisha imani ya umma kwa utoaji wa chanjo na kuhakikisha idadi kubwa yawa Australia wana chanjwa dhidi ya coronavirus.
Hata hivyo, miundombinu iliyopo ya zaidi yamaeneo 10,000 ya chanjo, na uwezo wakutoa dozi milioni tatu kila wiki inasalia. Idara ya Afya kwa sasa inasimamia mradi wakutoa chanjo, gazeti la.
Waziri Mkuu Anthony Albanese anatarajiwa kusimamia mkutano wa mtandaoni wa baraza lamawaziri lakitaifa Alhamisi.
Waziri Afya Mark Butler ame eleza bunge kuwa hivi karibuni Australia inaweza kuwa na mpango wakitaifa wakukabiliana na madhara ya muda mrefu ya UVIKO. Alisema kuwa serikali kwa sasa inatafuta ushauri wa wataalam.
Bw Butler amesema takriban asilimia nne ya wagonjwa wa UVIKO-19 hupitia uzoefu wa muda mrefu wa dalili.
Serikali ya shirikisho imetangaza msaada wa ziada kwa mradi wa Disability Support for Older Australians (DSOA). Serikali imesema mradi wa DSOA unaweza zingatia uwekezaji wa mara moja tu kwa wateja wanao athiriwa moja kwa moja na UVIKO-19 baada ya 1 Januari 2022.
Find a COVID-19 testing clinic
Register your RAT results here, if you're positive
Kama unahitaji msaada wakifedha, tazama maamuzi yako ni yapi.
Hapa kuna msaada wakuelewa lugha inayo tumiwa kuhusu UVIKO-19 katika lugha yako.