- Serikali ya shirikisho yatoa mradi mpya wa chanjo kwa wa Australia wa Kwanza.
- Queensland kuweka zahanati za chanjo katika fukwe
- Victoria yatoa mpango wake wakufungua jimbo kwa kiwango cha 90% ya chanjo
Victoria
Victoria inaratajiwa kufikisha lengo ya kiwango cha 80% ya chanjo wikendi ijayo. Uhuru wakusafiri jimboni humo utaanza Ijumaa 29 Oktoba.
Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema kuwa Victoria inatarajia kutoa kiwango cha 90% ya chanjo, kwa umma wenye miaka 12 na zaidi kufikia 24 Novemba.
Bw Andrews aliongezea kuwa, "Hii inamaana kwamba, hapatakuwa vikomo popote, hapatakuwa maswali ya wingi popote."
Hata hivyo, masharti ya dozi mbili ya chanjo yata endelea kufuatiliwa.
"Uchumi wa chanjo hauendi popote," alisema kiongozi wa jimbo.
Jimbo hilo limerekodi kesi mpya 1,935 ndani ya jamii pamoja na vifo 11.
New South Wales
New South Wales imerekodi kesi mpya 296 za maambukizi ndani ya jamii, pamoja na vifo vinne.
Jimbo hilo limetoa zaidi ya 84% ya chanjo kwa umma wenye zaidi ya miaka 16.
Serikali ya jimbo imezindua kampeni mpya kwa jina la 'Feel New South Wales' kukuza utalii baada ya jimbo hilo kufunguliwa tena.
Queensland
Queensland haija rekodi kesi yoyote leo.
Serikali ya jimbo inashirikiana na shirika la Surf Lifesaving Queensland kuweka zahanati katika fukwe za jimbo hilo katika wikendi ijayo.
Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- ACT imerekodi kesi mpya 9 ndani ya jamii.
- Serikali ya shirikisho imetoa kampeni mpya ya chanjo kwa jina la 'sambaza uhuru' pamoja na kampeni inayo lenga jamii yawa Australia wa kwanza kwa jina la 'sisi sote', kati ya wasiwasi kuhusu viwango vidogo vya chanjo miongoni mwa wa Australia wa kwanza.
- 86% yawa Australia kwa sasa wamepokea dozi yao ya kwanza ya chanjo, wakati idadi hiyo inaendelea kusalia kuwa 60% kwa wa Australia wa kwanza.
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: