Jumanne, Australia iliripoti vifo 53 vya UVIKO-19, vifo 28 viliripotiwa jimboni Victoria na vifo saba viliripotiwa jimboni New South Wales. Jimbo la Magharibi Australia nalo liliripoti vifo sita vyakihistoria.
Majimbo ya NSW na Queensland yaliripoti kesi 1,499 na idadi yawatu 491 ambao wana UVIKO-19 wamelazwa hospitalini, hiyo ikiwa ni idadi kubwa ya watu ambao wamelazwa hospitalini katika wiki nne zilizopita.
Tazama matukio mapya ya UVIKO-19 kwa kesi mpya, wanao lazwa hospitalini na vifo nchini Australia .
Moderna inatarajiwa kuanza majaribio ya mchanganyiko wa chanjo ya mafua na UVIKO-19 baadae mwaka huu.
Kampuni hiyo ya madawa inaweza zalisha chanjo moja katika kiwanda chake jimboni Victoria. Wa Australia wanaweza pata chanjo hiyo kufikia mwaka wa 2024.
Watafiti katika chuo cha Adelaide wana anza majaribio kwa binadam, kwa chanjo mpya ya jeki ya UVIKO-19 ambayo silazima kutumia sindano wiki hii. Chanjo hiyo inayo husu DNA, imeundwa kulenga aina yakirusi cha Omicron. Chanjo ya sasa imeidhinishwa kwa matumizi nchini Australia, inalenga aina ya asili ya kirusi hicho.
Mamlaka yabidhaa na madawa ya Australia almaarufu (TGA) ina tathmini pendekezo kutoka kampuni ya Moderna, kwa kuruhusu matumizi ya chanjo ya UVIKO-19 katika watoto wenye chini ya miaka tano. Hata hivyo, TGA inaweza chukua wiki kadhaa kabla yakufanya maamuzi.
Kituo cha udhibiti wa magonjwa nakuzuia cha Marekani, hivi karibuni kili idhinisha chanjo ya UVIKO-19 kwa watoto ambao wanachini ya miaka tano.
Serikali ya chama cha Labor inatarajiwa kutangaza tume yakifalme au, uchunguzi mwingine kwa jinsi Australia imesimamia janga la UVIKO-19 baada ya majira ya baridi.
Jimbo la Kusini Australia hivi karibuni linaweza inua amri ya chanjo tatu, kwa wafanyakazi wa huduma za afya, watalaam wanao tibu miguu, wataalam wa matibabu ya viuongo, wataalam wanao wasaidia watu kushiriki katika shughuli za kila siku pamoja na watalaam wanao tibu majeraha.
Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya