Kundi la Ushauri la Australia la ufundi kuhusu chanjo (ATAGI) lina fanya tathmini ya ushahidi kwa chanjo ya Comirnaty (Pfizer), kabla chanjo hiyo iidhinishwe kutolewa kama chanjo ya jeki katika vijana wenye kati ya miaka 12 hadi 15.
ATAGI imewahamasisha wazazi wa watoto wenye miaka kati ya 5 hadi 11, waombe miadi ya dozi yao ya pili ya chanjo ya UVIKO-19.
Mweka hazina wa NSW Matt Kean jana Jumatatu alipatwa na UVIKO-19.
Kiongozi wa Victoria, Daniel Andrews anajitenga kwa muda wa siku saba baada ya kipimo chake cha rapid antigen cha uviko kurejesha matokeo chanya.
Kuna uwezekano Magharibi Australia inaweza shusha hatua za 'Kiwango cha 2' hadi 'Kiwango cha 1' kuanzia saa sita dakika moja usiku wa Alhamis 31 Machi, licha ya ongezeko ya kesi mpya za UVIKO tangu 7 Machi ambapo jimbo hilo limerekodi maambukizi 2,365. Jimbo hilo lilifikia kilele cha maambukizi mapya 24 Machi baada yakurekodi kesi mpya 8,616 za maambukizi.
Sharti lakuvaa barakoa kwa watu wenye miaka 8 na zaidi lita endelea (pamoja na wanafunzi wa darasa la 3 na juu shuleni) katika sehemu ambazo si nyumbani kwa wahusika Magharibi Australia. Bonyeza kwa taarifa zaidi.
Profesa Catherine Bennett, ni Mwenyekiti wa masomo yakudhibiti magonjwa katika Chuo cha Deakin, ameonya kuhusu kutegemea sana vipimo vya RAT, kwa sababu ya maswala ya usahihi. Amesema usahihi wa vipimo vya RAT unatofautiana katika nyumba tofauti. Kwa mfano, matokeo yanaweza tofautiana kama watu walitumia chakula au, walipiga mswaki nusu saa kabla yakufanya kipimo hicho.
Takwimu za UVIKO-19 Australia kwa 29 Machi 2022
New South Wales: Kesi mpya 21,494, wagonjwa 1,283 hospitalini, wagonjwa 53 wako ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti, vifo tisa
Victoria: kesi mpya 10,916, wagonjwa 284 hospitalini, wagonjwa 33 wako ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti, vifo tano
Tasmania: kesi mpya 2,324, wagonjwa 22 wako hospitalini, hakuna mgonjwa yeyote katika kitengo cha wagonjwa mahtuti, kifo kimoja
Queensland: kesi mpya 7,738, wagonjwa 325 wako hospitalini, wagonjwa 14 wako ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti, vifo tisa
Australian Capital Territory: kesi mpya 1,063, wagonjwa 49 wako hospitalini, wagonjwa wanne wako ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti, hakuna vifo vyovyote
Northern Territory: kesi mpya 408, wagonjwa 12 wako hospitalini, wagonjwa wawili wako ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti, hakuna vifo vyovyote
South Australia: kesi mpya 4,201, wagonjwa 170 wako hospitalini, wagonjwa saba wako ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na kifo kimoja
Western Australia: kesi mpya 8,910, wagonjwa 219 wako hospitalini, wagonjwa sita wako ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na kifo kimoja
Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19 hapa
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya