- Jimboni NSW, 67% yawakaaji wamepokea dozi yao ya kwanza ya chanjo
- Jimbo la Victoria lina zaidi ya maeneo 1,000 ya maambukizi ya COVID-19
- Wilaya ya ACT imeongeza muda wa makatazo hadi 17 September
- Jimbo la SA lainua vizuizi kwa wasafiri kutoka Wilaya ya Kaskazini na Queensland
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 1,164 zamaambukizi ndani ya jamii, kesi 796 zikiwa katika maeneo ya Magharibi na Kusini Magharibi Sydney. Watu watatu walifariki.
Afisa Mkuu wa Afya wa jimbo hilo Dr Kerry Chant ame wahamasisha wakaaji wa vitongoji vya Guildford, Merrylands, Auburn, Greenacre, Bankstown na Blacktown wakapimwe.
Waziri wa Afya wa NSW Brad Hazzard ame shauri mtu yeyote ambaye ana zaidi ya miaka 18, apate chanjo ya AstraZeneca kwa sababu hakuna chanjo zakutosha za Pfizer.
Mwanaume mmoja waki Aboriginal mjini Dubbo, alitangazwa Jumatatu kama mtu wakwanza kufa, kwa sababu ya COVID-19 katika mlipuko wa sasa katika eneo la Magharibi ya New South Wales.
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 76 ndani ya jamii, zikijumuisha kesi 31ambazo bado hazija ungwa na milipuko ya sasa.
Kiongozi wa jimbo hilo Andrews, ambaye ata tangaza mpango wakuregeza vizuizi kesho, amesema 'chanjo sahihi ni ile ambayo unaweza pata', akidokeza kuhusu upatikanaji kwa wingi wa dozi za chanjo za AstraZeneca.
Kwa sasa kuna zaidi ya sehemu 1,000 , ikijumuisha majengo kadhaa mjini Melbourne.
Australian Capital Territory
Wilaya ya The ACT imerekodi kesi mpya 13 ndani ya jamii, angalau kesi nane zikiwa zilikuwa ndani ya jamii zilipokuwa katika hali ambukizi.
Zahanati ya watu wengi ya chanjo za COVID-19 mjini Canberra, itafunguliwa katika ukumbi wa Taasisi ya Michezo ya Australia Ijumaa, 3 Septemba. Muda wa makatazo ume ongezwa hadi 17 Septemba, vizuizi .
Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- Kusini Australia yainua vizuizi vyote kwa watu wanao safiri kutoka Kusini Mashariki Queensland na Katherine katika Wilaya ya Kaskazini.

Source: ALC
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: