- NSW yapanua malipo ya msaada wa COVID-19
- Victoria yatangaza uwekezaji wa ziada kwa msaada wa afya ya akili
- Makatazo jimbo la ACT yaongezwa hadi 15 Oktoba
- Queensland yarekodi kesi moja mpya ndani ya jamii
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 1,127 ndani ya jamii pamoja na vifo viwili.
Baada ya kutambuliwa kwa kisa cha COVID-19 jana katika eneo la halmashauri la Yass Valley, amri zakubaki nyumbani zita tumiwa kwa kila mtu anaye ishi au aliyekuwa katika eneo hilo tarehe 9 Septemba au baada ya tarehe hiyo.
NSW Health imewahamasisha wakaaji wa Young ambayo iko katika eneo la wilaya ya afya ya Murrumbidgee wajitokeze kufanyiwa vipimo, baada ya virusi hivyo kutambuliwa katika kiwanda cha taka. Kabla ya tukio hilo, palikuwa hapa jakuwa kesi yoyote katika jamii hiyo.
yame panuliwa kwa wafanyakazi na jamii ambazo ziko katika hali mbaya, misaada hiyo inajumuisha uwekezaji kwa makundi yenye lugha na tamaduni mbali mbali.
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 445 ndani ya jamii, pamoja na vifo viwili. Jimbo hilo kwa sasa lina shughulikia kesi 3,799, wakati 85% yao wana umri wa chini ya miaka 50.
Naibu kiongozi wa jimbo hilo James Merlino ametangaza mfuko wa uwekezaji wa dola milioni 22.1 kuunda huduma ya afya ya akili ndani ya jamii katika kanda ya Victoria na, maeneo ya jiji la Melbourne.
Australian Capital Territory
Wilaya ya ACT imerekodi kesi mpya za maambukizi 22 ndani ya jamii.
Makatazo katika wilaya hiyo yata ongezwa kwa muda wa wiki nne, mageuzi ya ziada kwa vizuizi yakitarajiwa kuanzia tarehe 17 Septemba, baadhi ya mageuzi hayo yakijumuisha biashara ndogo kuruhusiwa kuwadumia watu watano ndani ya biashara hiyo wakati wowote au, mtu mmoja kuwa na umbali wa mita nne na mteja mwenza ndani ya biashara husika.
Bonyeza hapa kutazama ustahiki wako kwa au kuona .
Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- Wakaaji wa Magharibi Australia wenye umri wa miaka 60 na zaidi, wata stahiki kupewa chanjo ya COVID-19 ya Pfizer kuanzia wiki ijayo.
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: