Jumanne, Australia iliripoti vifo 70 vya UVIKO-19, vifo 40 viliripotiwa New South Wales (NSW), 19 Queensland na 11 Victoria. Pia Magharibi Australia iliripoti vifo vinne vyakihistoria.
Wilaya ya Australian Capital Territory (ACT) inaendelea kurekodi idadi kubwa zaidi ya watu wanao lazwa hospitalini tangu janga hili lilipo anza. Wilaya hiyo iliripoti kuwa idadi ya watu 121 wenye UVIKO-19, walilazwa hospitalini kulinganisha na Jumatatu ambako watu 119 wali lazwa hospitalini.
Mamlaka wa afya wa ACT wana chunguza mlipuko wa UVIKO-19 katika wodi ya saratani ndani ya hospitali moja ya Canberra. Wodi hiyo imefungwa kwa mapokezi mapya ya wagonjwa, hadi mlipuko huo utakapo dhibitiwa.
Queensland inaendelea kupitia uzoefu wa ongezeko kubwa katika idadi ya wanao lazwa hospitalini. Jumanne, jimbo hilo liliripoti idadi ya watu 593 ambao wana UVIKO-19 ambao wamo hospitalini, ambayo ni idadi kubwa zaidi katika muda wa miezi mbili iliyopita.
John Gerrard ni afisa mkuu wa afya, alieleza shirika la habari la kuwa wimbi jipya lina gonga jimbo hilo kwa ongezeko ya kesi za virusi vya BA.5 na BA.4. Amesema kesi za virusi vya BA.5 na BA.4, ni 38% ya kesi mpya kulinganisha na chini ya 2% ya wiki nne zilizo pita.
Bw Gerrard alihamasisha wakaaji wanaostahiki wachukue dozi zao za jeki za tatu naza nne, wakati kuna matarajio ya ongezeko ya wanao lazwa hospitalini. Aliomba pia wakaaji wa Queensland, wachunguze ustahiki wao kwa dawa zakinga ya UVIKO-19.
Utafiti uliofanywa na kituo cha taifa kwa utafiti wa chanjo na ufuatiliaji (NCRIS) umeonesha kuwa chanjo ya jeki ya au dozi ya tatu ya UVIKO-19, hutoa 65% ya ulinzi zaidi dhidi yakulazwa hospitalini au kifo kutoka kwa virusi vya Omicron kuliko aliye pokea dozi mbili za chanjo.
Utafiti huo ulifanywa wakati wa kilele cha wimbi la virusi vya Omicron katika mwezi wa Januari na Februari 2022 nchini Australia.
Matokeo ya Sensa ya 2021 yaliyo chapishwa mapema leo Jumanne, yalionesha kupungua kwa mapokezi ya wahamiaji wapya katika miaka ya janga ya 2020 na 2021.
Data inaonesha kuwa idadi ya watu 165,000 waliwasili nchini kati ya mwaka wa 2020 na 2021, kulinganisha na zaidi ya idadi ya watu 850,000 walio wasili nchini kati ya miaka ya 2017 na 2019.
Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya