Jumanne, Australia iliripoti vifo 52 vya UVIKO-19, 20 vikiwa Victoria, 16 New South Wales na vifo 12 Queensland.
Idadi ya wanao lazwa hospitalini imekuwa ikiongezeka katika eneo la Australian Capital Territory, tangu 4 Aprili. Wilaya ya ACT iliripoti kuwa watu 80 walikuwa wamelazwa hospitalini siku ya Jumanne.
Tazama maendeleo kwa kesi mpya za UVIKO-19, takwimu za wanao lazwa hospitalini na vifo nchini Australia .
Watu wa karibu wa walio ambukizwa Uviko-19 katika jimbo la Magharibi Australia, wanaweza chukua kipimo chao cha aina ya rapid antigen bure, katika vitongoji vya Joondalup, Jandakot na Bassendean kuanzia 18 Mei.
Jimbo la Kusini Australia kufungua vituo 40 vya chanjo katika mashule kuanzia, 27 Mei kupiga jeki viwango vya chini vya chanjo miongoni mwa watoto wenye miaka 5 hadi 11. Mradi huo wa chanjo utatumiwa katika shule 10, kila Ijumaa na Jumamosi ya wiki.
Afisa Mkuu wa afya wa Kusini Australia Nicola Spurrier, amesema watoto tisa jimboni humo wamepata magonjwa mabaya (PIMS-TS) tangu mwanzo wa janga hili.
Profesa Spurrier amesema PIMS-TS, ni ugonjwa usio wa kawaida na unaweza kuwa tisho kwa maisha unao sababishwa na UVIKO-19, ila unaweza zuiwa kupitia chanjo.
Kundi lakiufundi la ushauri la Australia kwa maswala ya chanjo, linafanyia ushahidi tathmini kama dozi za chanjo, zinahitajika kwa watoto wenye miaka kati ya 12 hadi 15, watoto ambao wana magonjwa sugu wakijumuishwa.
Pata zahanati ya kupimia UVIKO-19
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya