Taarifa mpya ya UVIKO-19: Vifo 52 vyaripotiwa Australia; ongezeko ya watu wanao lazwa ACT

Hii ni taarifa yako mpya kuhusu UVIKO-19 nchini Australia kwa 31 Mei 2022.

Leading epidemiology modellers predict another COVID wave in early June.

Leading epidemiology modellers predict another COVID wave in early June. (file) Source: AAP Image/Brendon Thorne

 

Jumanne, Australia iliripoti vifo 52 vya UVIKO-19, vifo 20 vikiwa Victoria, 19 New South Wales (NSW) na 11 Queensland (QLD). katika nyongeza jimbo la Magharibi Australia liliripoti vifo 4 vyakihistoria.

Kulinganishwa na siku iliyopita, kulikuwa ongezeko ya idadi mpya ya maambukizi ya UVIKO-19 yaliyo ripotiwa, pamoja na idadi yawatu wanao lazwa hospitalini kote Australia.  

Wilaya ya The Australian Capital Territory (ACT0 iliripoti idadi ya watu 93 walio lazwa hospitalini wakiwa na UVIKO-19, idadi kubwa zaidi tangu 4 Aprili. 

Tazama mitindo mipya ya UVIKO-19 kwa kesi mpya, visa vya wanao lazwa hospitalini pamoja na vifo nchini Australia .


Waundaji wakuu waelimu ya milipuko ya magonjwa wametabiri wimbi lingine la UVIKO katika mwezi wa Juni. Ripoti katika  iliwanukuu watalaam wa milipuko ya magonjwa waliosema, maambukizi yanayo sababishwa na aina ya BA.2 ya Omicron yametulia nchini, na aina mpya ya maambukizi ya BA.4 na BA.5 yataongeza maambukizi mapya.

Victoria imetangaa itatoa chanjo za mafua bure kwa wakaaji baada ya kesi kuongezeka kwa zaidi ya 30% katika wiki iliyo pita. Chanjo hizo bure zitatolewa katika zahanait 3,000 zama GP na katika duka zamadawa za jamaii kati ya 1 na 30 Juni.   

Majimbo ya NSW, SA na QLD tayari yametangaza yata toa chanjo bure zamafua kwa wakaaji wao.

Jimbo la SA limetangaza kesi ya ugonjwa wa meningococcal baada ya mvulana mwenye miaka 13, kulazwa hospitalini. Watu wanane wakaribu yake wameshauriwa wakachukue dawa.

Ugonjwa huo wabakteria unaweza kuwa mubaya, unaweza sababisha maambukizi katika ubongo, utiwamgongo na katika damu.

Japan kuruhusu watalii kutoka nchi 98 kuanzia 10 Juni, baada ya nchi hiyo kufungwa kwa sababu ya janga kwa miaka mbili. Hata hivyo, watalii wanaweza tembelea tu Japan kama sehemu ya vikundi vya watalii. 

 


 




Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19

Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya 



Kama unahitaji msaada wa fedha, 

Hapa kuna msaada waku saidia kuelewa 



Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika Kiswahili kwenye.  


Share
Published 31 May 2022 2:15pm
Presented by Gode Migerano


Share this with family and friends