Katika taarifa hii:
Chanjo ya COVID-19 nchini Australia
Serikali ya Australia ime ahidi kuwapa wa Australia wote, chanjo salama na fanisi ya COVID-19, punde itakapo patikana.

COVID-19 vaccine national roll-out strategy Source: Australian Government - Department of Health
Kama una miaka 40 au zaidi, una stahiki kuchanjwa. Kama una kati ya miaka 16 na 39, inawezekana unastahiki pia kuchanjwa. Fuata hatua kwenye tovuti hii, kujua kama unastahiki kupata chanjo.
Unaweza omba miada pia na GP wako na, kupewa taarifa kuhusu chanjo katika lugha yako:
Ni chanjo gani zinapendekezwa?
Kundi la ushauri lakiufundi kwa kwanjo nchini Australia (ATAG) limependekeza chanjo ya COVID-19 Comirnaty (Pfizer) kama chanjo inayo pendelewa kwa watu wenye kati ya miaka 16 na 56.
Chanjo ya COVID-19 AstraZeneca, nayo inaweza tolewa kwa watu wenye kati ya miaka 18 hadi 59.
Kama haustahiki na una miaka 18 au zaidi, unaweza omba ujulishwe utakapo stahiki.
Watu ambao wana chini ya miaka 16 bado hawastahiki kuchanjwa nchini Australia.
Msaada wa afya ya akili unao husiana na Covid-19
Mnamo mwaka wa, serikali ya Australia iliongeza huduma 10 zakisaikolojia za ruzuku ya Medicare katika kila mwaka, kwa wagonjwa wanao stahiki chini ya kwa jina la Upatikanaji Bora kwa wanasaikatria, wanasaikolojia nama GP kupitia mfumo wa .
Serikali ya Australia ime toa msaada wa huduma ya afya ya akili unao husiana na COVID-19, kupitia tovuti ya afya ya akili kwa jina la "" kutoa taarifa na mwongozo kwa jinsi yakuendelea kuwa na afya nzuri ya akili wakati wa janga la coronavirus nakujitenga.
ni mradi unao simamiwa na shirika la Mental Health Australia, liki lenga afya ya akili ya watu kutoka mazingira ya lugha na tamaduni mbali mbali (CALD), kutoa upatikaniji kwa rasilimali, huduma na taarifa katika hali nzuri yakitamaduni.
Uki hitaji msaada wa afya ya akili katika lugha yako, pigia simu shirika la TIS National kwa namba hii 131 450 au tembelea tovuti hii kupata mkalimani. Shirika la TIS National hufanya kazi katika zaidi ya lugha 100 na, huduma zake zinapatikana masaa 24 kwa siku, siku 7 za wiki, kwa gharama ya simu ya kawaida nchini.
Tembelea kwa taarifa zaidi kuhusu huduma za afya ya akili.
Financial difficulties (Malipo ya Maafa ya Likizo ya Janga)
Kama unakabiliwa na matatizo yakifedha nenda kwa au pigia simu namba ya msaada yakitaifa yamadeni 1800 007 007.
Malipo hayo yanatolewa kwa wafanyakazi ambao hawa wezi pokea mapato kwa sababu, lazima wajitenge au waingie katika karantini, au lazima watoe huduma kwa mtu ambaye ana COVID-19.
Bonyeza viunganisho hapo chini, kupata taarifa kuhusu Likizo ya Janga, katika kila jimbo na mkoa:
Je COVID-19 inaeneaje na unaizuiaje?
COVID-19 inaenea kutoka kwa mtu hadi kwa mtu kupitia:
- Kuwasiliana kwa karibu na mtu wakati anaambukiza hata kabla ya dalili zao kuonekana.
- Kukaa karibu sana na mtu aliye na maambukizi aliyethibitishwa ambaye hukohoa au kupiga chafya.
- Kugusa vitu au nyuso (kama vile vipuli vya mlango au meza) vilivyochafuliwa kutokana na makohozi au kupiga chafya kutoka kwa mtu aliye na maambukizi yaliyothibitishwa, kisha kugusa mdomo wako au uso.
Unaizuia kwa kuzoea kuweka mikono safi na kupiga chafya vizuri/kukohoa na kujiweka mbali kutoka kwa wengine unapokuwa mgonjwa ni njia bora ya kujilinda dhidi ya virusi vingi. Unapaswa:
- Endelea kuzingatia kutokuwa karibu na wengine kwa takribani mita 1.5 na zingatia sheria ya mtu 1 kwa mita za mraba 4.
- Osha mikono yako mara kwa mara na sabuni na maji, kabla na baada ya kula, na baada ya kwenda choo.
- Funika kikohozi chako na kupiga chafya, toa tishu, na utumie vitakasa mikono vinavyotokana na pombe.
- Ikiwa haujiskii vizuri, epuka kukutana na wengine (kaa zaidi ya mita 1.5 kutoka kwa watu).
Ukionyesha dalili, nenda kapime
Dalili za Virusi vya Corona zinaweza kuanzia kutoka ugonjwa mdogo hadi pneumonia, kwa mujibu wa tovuti ya Serikali ya Shirikisho.
Dalili za COVID-19 ni sawa na zile zingine za homa na mafua na ni pamoja na:
- Homa
- Kuwashwa kwa koo
- Kikohozi
- Uchovu
- Ugumu wa kupumua
Dalili zingine zinaweza jumuisha, kutokwa na makamasi, kichwa kuuma, maumivu ya misuli au viungo, kichefuchefu, kuharisha, kutapika, kukosa uwezo wa kutambua harufu, mabadiliko ya kutambua ladha, kukosa hamu ya kula na uchovu.
Mamlaka imetengeneza mfumo wa kuangalia Dalili za COVID19 ambao unaweza kuutumia ukiwa nyumbani:
Hakuna matibabu maalumu ya ugonjwa wa virusi vya corona, lakini dalili nyingi zinaweza kutibiwa kwa msaada wa matibabu. Dawa za viuadudu hazifanyi kazi dhidi ya virusi.
Ikiwa unapata dalili, unatakiwa upimwe.
Ikiwa unataka kuzungumza na mtu kuhusu dalili zako, piga simu kwa Msaada wa kitaifa wa virusi vya Corona kupata ushauri. Simu yao hufanya kazi masaa 24 kwa siku, siku saba za wiki: 1800 020 080
Tafuta ikiwa kuna karibu na eneo lako na jinsi ya kujiandikisha kwa miadi.
Ikiwa unahangaika kupumua au una dharura ya matibabu, piga simu 000.
[sbsondemand
Unaweza kupimwa wapi?
Bonyeza viunganisho hapa chini kufahamu kliniki za upimaji katika jimbo na kitongoji chako:
Ikiwa umegunduliwa na COVID-19, lazima ujitenge mwenyewe:
- usiende kwenye maeneo ya umma kama vile kazini, shuleni, vituo vya ununuzi, chekechea au chuo kikuu
- muulize mtu akuletee chakula na mahitaji mengine na waviache kwenye mlango wako wa mbele
- usiruhusu wageni ndani - il tu watu ambao kawaida wanaishi na wewe wanapaswa kuwa nyumbani kwako
Ni nani aliye katika hatari kubwa ya kuumwa sana?
Watu wengine ambao wameambukizwa wanaweza kukosa kuwa wagonjwa, wengine watapata dalili kali ambapo watapata nafuu kirahisi, na wengine wanaweza kuwa wagonjwa sana, kwa haraka sana. Kutoka kwa uzoefu wa zamani na magonjwa mengine, watu walio kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa vibaya ni:
- Waaborigino na watu wa visiwani Torres Strait, wenye umri zaidi ya miaka 50 na wazee walio na moja au magonjwa zaidi sugu
- Watu wenye miaka 65 na wazee walio na hali ya magonjwa sugu. Magonjwa hayo yanajumuisha kwa tafsiri ya 'magonjwa sugu' itafafanuliwa kadri ushahidi zaidi unavyoibuka.
- Watu wenye umri wa miaka 70 na wazee
- Watu walio na kinga dhaifu
Wajibu wako ni nini ikiwa umegunduliwa na COVID-19?
Ikiwa umegunduliwa na COVID-19, lazima ujitenge mwenyewe:
- usiende kwenye maeneo ya umma kama vile kazini, shuleni, vituo vya ununuzi, chekechea au chuo kikuu
- muulize mtu akuletee chakula na mahitaji mengine na waviache kwenye mlango wako wa mbele
- usiruhusu wageni ndani - il tu watu ambao kawaida wanaishi na wewe wanapaswa kuwa nyumbani kwako
Je! Napaswa kuvaa barakoa?
Baadhi ya majimbo na vitongoji vya Australia vinashauri au vinahimiza matumizi ya uvaaji barakoa.
Ikiwa hali itabadilika katika jimbo au kitongoji chako hivyo ushauri wa barakoa unaweza kubadilika. Ni muhimu kupata taarifa mpya za ushauri katika eneo lako.
Ili kuendelea kupata ushauri wa hivi karibuni kuhusu barakoa, fuata vielelezo vipya vya serikali za mitaa:
Unapovaa barakoa, ni muhimu kuivaa vizuri:
• osha au safisha mikono yako kabla ya kuivaa au kuivua
• hakikisha barakoa inafunika pua yako na mdomo na inatoshea vizuri chini ya kidevu chako, juu ya pua yako na pande za uso wako
• usiguse sehemu ya mbele ya barakoa yako ukivaa au ukiondoa
• usiruhusu barakoa kutundika shingoni mwako au chini ya pua yako
• usitumie tena barakoa ya matumizi mara moja; osha na kausha barakoa inayoweza kutumika tena baada ya matumizi na uhifadhi mahali safi kavu.
Kusafiri kutoka au kuingia ndani ya Australia
Majimbo na vitongoji vinaweza kutumia vizuizi vyake, ikijumuishwa kufunga mipaka yao ya jimbo.
Ukusanyaji wa lazima wa data
Kuanzia 1 Oktoba 2020, kuna ukusanyaji wa lazima wa data kwa ndege za ndani kusaidia majimbo na wilaya linapokuja suala la kutafuta walioambukizwa: jina, anwani ya barua pepe, nambari ya mawasiliano ya mkononi, na jimbo la makazi.
Kanuni za Kitaifa za Usafiri wa Umma
Huduma za usafiri wa umma ni jukumu la majimbo na vitongoji, na Baraza la Mawaziri la Kitaifa limeweka kanuni kadhaa za kusaidia kudhibiti afya na usalama wa wafanyakazi na abiria kwenye vyombo vya usafiri wa umma, pamoja na: kutosafiri wakati ukijihisi kuumwa, kuzingatia umbali kutoka kwa madereva na abiria wengine, na epuka kutumia pesa taslimu.
Vikwazo vya kusafiri
Kuna hatua za muda mfupi kwa safari za kimataifa ambazo mara kwa mara hupitiwa upya.
Hii inaweza kuathiri safari yako kuingia Australia. Taarifa zinabadilika mara kwa mara, kwa maelezo zaidi tembelea:
Mahitaji ya karantini na kupima yanasimamiwa na kutekelezwa na serikali za majimbo na vitongoji:
- NSW and
- VIC , and
- ACT and
- NT and
- QLD and
- SA and
- TAS and
- WA and
Ikiwa unataka kusafiri ng'ambo, unaweza kuomba mtandaoni kusamehewa kwa dharura kusafiri ikiwa utakuwa chini ya moja ya makundi yafuatayo:
- kusafiri kwako ni kama sehemu ya muitikio wako kwa mlipuko wa COVID-19, pamoja na utoaji wa misaada
- kusafiri kwako ni muhimu kwa mwenendo wa viwanda muhimu na biashara (pamoja na viwanda vya usafirishaji nje na uagizaji)
- unasafiri kupata matibabu ya haraka ambayo hayapatikani nchini Australia
- unasafiri kwa biashara binafsi ya haraka na isiyoweza kuepukika
- misaada au misingi ya kibinadamu
- kusafiri kwako ni kwa faida ya kitaifa.
kwa taarifa zaidi kuhusu masharti ya kuondokaAustralia.
- Ili kujua jinsi gani Serikali ya Australia inasimamia janga la COVID-19, tembelea, .
- Maelezo zaidi kwa lugha ya kiingereza tembelea .
- Idara ya mambo ya ndani - maelezo kwa jamii za Waustralia kupitia .
- Watu nchini Australia lazima wakae umbali wa mita 1.5 kutoka kwa mwingine. Angalia vizuizi vya makutano katika jimbo lako.
- Ikiwa unajihisi na dalili za homa au mafua, kaa nyumbani na panga hatua za upimaji kwa kumpigia daktari wako au kuwasiliana na namba ya watoa huduma za maelezo ya afya kitengo cha virusi vya corona kupitia 1800 020 080.
- Habari na maelezo yanapatikana kwa lugha 63 kupitia
- Tafadhali angalia miongozo kwa jimbo au mkoa wako: , , , , , , .