Wapiga kura walipo wasili katika vituo vyakupiga kura, maafisa wa uchaguzi walitazama kama wako katika sajili yakupiga kura, na punde baada ya uthibitisho huo walipewa karatasi yenye ambayo ilikuwa na swali moja lakujibu.
Swali hilo lilikuwa: “Pendekezo la Sheria: kubadili Katiba kuwatambua wa Australia wa Kwanza kwa kuanzisha Sauti yawa Aboriginal na wana visiwa wa Torres Strait. Una idhinisha badiliko hili lililo pendekezwa?”
Kufikia sasa tume ya uchaguzi ya Australia (AEC) imechapisha matokeo yafuatayo 60.25% ya kura, wakati kampeni ya NDIO imepata 39.75%.
Takwimu zote pia zina onesha kuwa majimbo yote pamoja na wilaya ya Northern Territory yamepiga kura ya LA, wilaya ya ACT pekee ndiyo iliyopiga kura ya NDIO kwa wingi.
Tuta waletea taarifa zaidi kuhusu kura hiyo punde tutakapo zipata.