Key Points
- New COVID cases continue to drop in NSW and VIC
- Australia to monitor travellers from China but no measures at this point in time
- Authorities encourage COVID-safe plan for NYE
New South Wales ilirekodi idadi nyingine ndogo ya kesi mpya za UVIKO wiki hii, kesi mpya 27,665 ziliripotiwa ambazo ni chini ya kesi 38,610 zilizo ripotiwa wiki jana.
Vifo vinavyo sababishwa na UVIKO navyo vilipungua sana jimboni humo, idadi ya vifo 32 viliripotiwa, kulinganisha na vifo 78 wiki iliyopita.
Vivyo hivyo, Victoria ilishuhudia kupungua kwa kesi mpya za UVIKO pamoja na vifo vinavyo sababishwa na UVIKO wiki hii.
Idadi ya kesi mpya 16,568 ziliripotiwa, kulinganisha na kesi 24,238 wiki iliyopita, na idadi ya vifo 69 viliripotiwa kulinganisha na idadi ya vifo100 wiki jana.
China itamaliza masharti yake ya karantini kwa wasafiri wanao wasili nchini humo kuanzia 8 Januari na ita anza kutoa pasi tena kwa wanao taka enda ng'ambo, licha ya ongezeko ya kesi za UVIKO nchini humo.
Marekani imeweka sharti la vipimo vya lazima vya UVIKO, kwa wasafiri wote kutoka China kuanzia 5 Januari, hatua hizo ziko tayari Japan, India, Italy na Taiwan.
Serikali ya Australia inaendelea "kufuatilia" hali hiyo na "itachukua hatua kwa mujibu wa ushauri wa afya", Waziri Mkuu Anthony Albanese alieleza kipindi cha Seven's Sunrise Alhamisi.
"Kwa sasa, hapajakuwa mabadiliko kwa ushauri wa usafiri kati ya China na Australia."
Afisa Mkuu wa matibabu Paul Kelly aliunga mkono uamuzi huo Alhamisi, akisema aina ya virusi vinavyo sababisha ongezeko ya maambukizi China, vime zunguka nchini Australia tayari.
Hata hivyo waziri kivuli wa uhamiaji, Dan Tehan ali eleza Radio National Ijumaa kuwa serikali inahitaji kuwa wazi kuhusu maamuzi yake, nakuomba ushauri wa matibabu uwekwe wazi.
"Moja ya vitu serikali ya zamani ilifanya ilikuwa kuhakikisha kwamba ushauri wa afya unatangulia; usalama wa wa Australia unapewa kipaumbele."
Tunapo elekea katika sherehe za mwaka mpya, mamlaka wana hamasisha watu wafanye hivyo wakiwa na mpango wa usalama wa UVIKO.
Jipimishe kama una dalili, jumuika nje au katika sehemu ambako hewa inapita vizuri, vaa barakoa au kuwa na moja karibu iwapo hauwezi kuwa mbali na wengine.
Hakikisha umepata chanjo zako zote na tazama kama unafuzu kupata dawa za uviko.
Kama hauwezi wasiliana na GP wako katika muda wa mwaka mpya, unaweza piga simu kwa namba yamsaada yakitaifa ya Coronavirus 1800 020 080.
Wako wazi masaa 24, siku 7 za wiki na wanaweza tazama kama unastahiki kupewa dawa hizo zakukabiliana na virusi.
Huduma zifuatazo za janga na taarifa, zinaweza patikana wakati wa likizo:
- – . Kwa watu ambao wana ulemavu wakusikia, tuma ujumbe mfupi wasimu kwa Lifeline kwenye namba hii 0477 131 144
- youth portal –
- Access Mental Health Team (pata huduma kwa timu ya afya ya akili)– or
- Suicide Call Back Service (huduma kwa simu kwa wenye wanataka jiua)–
Pata zahanati ya UVIKO
Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19
Sajili matokeo yako ya kipimo cha RAT hapa, kama ni chanya
Kuna msaada hapa waku kusaidia kuelewa ere is some help understanding