Feature

Australia imepiga kura ya 'La' katika kura ya maoni ya Sauti yawa Australia wa kwanza Bungeni

Pendekezo la Sauti kwa Bunge, lime shindwa katika kura ya maoni ya kwanza ya Australia katika zaidi ya miongo mbili.

Canva tile for FB.png
Key Points
  • The Indigenous Voice to Parliament referendum has resulted in a resounding 'No' vote.
  • Six states and the Northern territory recorded a 'No' vote, while the ACT voted 'Yes'.
  • Prime Minister Anthony Albanese urged Australians to come together.
LISTEN TO
INDIG REF 1410 UPDATED WRAP RNF image

Kura ya maoni ya Sauti yawa Australia wa kwanza bungeni ime isha kwa matokeo ya 'La'

SBS Swahili

07:36
Wa Australia wamekataa pendekezo la kuweka Sauti yawa Australia wa kwanza Bungeni ndani ya Katiba.

Kura ya 'La' ilirekodiwa katika majimbo yote sita pamoja na Northern Territory, katika kura hiyo ya maoni yakihistoria Jumamosi.

Kura ya 'La' inaongoza pia katika hesabu za jumla kitaifa.

ACT ndiyo mamlaka pekee iliyo rekodi kura ya 'Ndio' kwa wingi.

Waziri Mkuu Anthony Albanese aliye onekana kama mtu aliye kata tamaa, alisisitiza kuwa matokeo hayo "haya tufafanui na, hayata tugawanya".

"Sasa ni jukumu letu sote, kuja pamoja nakupata njia tofauti kwa safari ya maridhiano."
PM Anthony Albanese .jpg
Australian Prime Minister Anthony Albanese delivers a statement on the outcome of the Voice Referendum at Parliament House.
Kiongozi wa Upinzani Peter Dutton alihamasisha nchi iungane, akiongezea kuwa kura ya maoni ilikuwa zoezi ambalo Australia "haiku hitaji fanya".

"Pendekezo na mchakato huo ulistahili undwa kuwaunganisha wa Australia, si kutugawanya," alisema.
PETER DUTTON VOICE REFERENDUM ADDRESS
Opposition Leader Peter Dutton and Shadow Minister for Indigenous Australians Senator Jacinta Price address the media following the referendum. Source: AAP / JONO SEARLE/AAPIMAGE
Baadhi yawa Australia wakwanza wanachukua "wiki ya ukimya" kufuatia matokeo ya kura hiyo, wakati wengine tayari wanatazamia kitakacho fuata.

Waziri wa waAustralia wa kwanza ambaye pia alikuwa mwanaharakati wa kampeni ya 'Ndio' Linda Burney, amesema ana amini kuwa kizazi kipya cha viongozi wa waAustralia wa kwanza, wata ibuka kufuatia kura hii.

Mwanaharakati maarufu wa kampeni ya 'La' Nyunggai Warren Mundine amesema matokeo hayo yamedokeza kuwa wa Australia "wanataka vitu vifanywe" kuhusu maswala yanayo kabili jumuiya ya waAustralia wa kwanza.

"Watu wanastahili acha kufumbia macho vurugu, unyanyasaji, udhibiti wakulazimisha na, tabia zauharibifu zinazo endelea katika baadhi ya jumuiya zawa Australia wa kwanza," alisema.

Endelea kupata taarifa kuhusu kura ya maoni ya Sauti yawa Australia wa kwanza Bungeni kupitia mitandao ya SBS, pamoja na mitazamo yawa Australia wa kwanza kupitia NITV.

kupata makala ya maandishi, video, pamoja na makala yaliyo rekodiwa katika zaidi ya lugha 60, au fuatilia taarifa mpya na uchambuzi, pamoja nakupata burudani bure, kupitia tovuti ya

Share
Published 17 October 2023 1:22pm
Updated 17 October 2023 2:02pm
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends